Kikosi cha Yanga ambacho  jana kwa mara ya kwanza walivaa jezi za mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Vodacom, lakini zikiwa na alama nyeusi badala ya alama nyekundu. Katika mchezo huo Yanga  ililazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar na kuendelea kushika mkia kwenye msimamo wa ligi hiyo. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

Yanga wameendelea kung'ang'ania mkiani mwa Ligi Kuu huku mahasimu wao Simba wakipata ushindi wa tatu mfululizo kwenye ligi hiyo katika mechi zilizofanyika jana kwenye viwanja vya Jamhuri, Morogoro na Mkwakwani, Tanga.

Yanga walishuka kwenye Uwanja wa Jamhuri wakiwa na matumaini ya kupata pointi tatu, lakini walijikuta wakilazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar, wakati Gervas Kago alifunga bao lake la kwanza tangu aanze kuichezea Simba na kuiwezesha timu hiyo kuilaza Villa Squad bao 1-0, huku Polisi Dodoma wakitoka suluhu na Ruvu Shooting.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi tisa na kupanda hadi nafasi ya pili nyuma ya kinara wa ligi JKT Ruvu kwa tofauti ya mabao.



Mabingwa wa Kombe la Kagame Yanga waliokusanya pointi mbili katika michezo mitatu ya ligi waliyocheza mpaka sasa walilazimika kubaki ndani ya uwanja wa Jamhuri kwa dakika tano na kuondolewa na ulinzi mkali wa polisi FFU baada ya mashabiki wao wenye hasira kuanza kurushia mawe basi lililobeba wachezaji hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Kwama kweli hawapendi rangi nyekundu wangeanza ndani ya timu yao wenyewe kuziondoa, kama hapo kwenye kikosi chao wachezaji kama watano hivi wanaviatu vyenye rangi nyekundu kwenye mcahnganyo. huu ni ulimbukeni usio na elimu tu. wanakalia kuwaza mambo yasio na msingi na kusahau yalio na umuhimu. MAENDELEO YA MTANZANIA HAYACHELEWESHWI NA KINGINE ZAIDI YA UJINGA ALIONAO MTANZANIA MPAKA ANAFIKIA HATUA YA KUTOJITAMBUA. LAKINI ATAONGEA NA KUJITETEA KAMA VILE ANAJITAMBUA. sorry TZ.

    ReplyDelete
  2. Bwana Nditi asante. Ebu fuatilia huko TFF...Magazeti ya /Uhuru/Daily news/Mzalendo utuletee kumbukumbu ni Mwaka gani YANGA walishashika mkia kama sasa...Hali hii ilitokea Simba mwaka fulani..Wata-bounce back tu Yanga timu kubwa..YANGA KAMA ASENO!!

    David V

    ReplyDelete
  3. Kaaazi kweli kweli, huyo dogo aliyechuchumaa kavalishwa Yebo Yebo kudumisha utamaduni!!!!

    ReplyDelete
  4. Habari, wasomaji wa blog hii. Jamani hawa Yanga wamezidi, badala ya kubishana kwa nini wanafungwa/wanashidwa kushinda, wao wanagombana na rangi za jezi. Jamani watanzania, tunaenda wapi! Ifike basi wakati tuelimike. Mbona kwenye nchi za wenzetu viongozi wa timu huwa unatimuliwa, basi mi nashauri uongozi mzima wa Yanga uvunjwe na uundwe mwingine. Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  5. Hivi kwa nini yanga walikuwa wanakataa kuvaa jezi? Ni kwa sababu ya nembo kuwa Nyekundu?
    Hii ni kazi kweli kweli. Nembo inauhusiano gani na kucheza au u Yanga. Ningekuwa mimi ni vodacom ningetoa udhamini wangu kabisa. Ni ufinyu wa uelewa, na kupoteza muda kwa vitu vidogo vidogo. bado tunasumbuliwa na ushabiki wa miaka hiyooooooooooo!!!!!!!!!!!!!!!. Mimi ni yanga, lakini nisingepatwa na shida kuwa na kaalama kekundu kwenye jezi hata kidogo kwa sababu hako kaalama kameleta fedha na uwezo.
    Tuna safari ndefu sana.

    ReplyDelete
  6. Yanga mpaka sasa hamjamjua mchawi wenu! mchawi sio jezi bali maandalizi na kujipanga. Haya sasa jezi zimebadilishwa nembo nado mnafungwa sasa mtafute kisingizio kingine sio jezi.

    ReplyDelete
  7. Rangi nyekundu mguuni ni sawa kwani ni ya 'kukanyagwa' tuu...

    Mzozaji

    ReplyDelete
  8. Mabingwa wa kweli hata kama mtake msitake.. Mtabakia na ubao wenu!!

    ReplyDelete
  9. Full jezzy ni njano, logo tu wanagoma, yanga na hasa viongozi wao wamekaa kimtaani mno, hawafikiriii kabisa au wanamasubuni mno! wanakataa logo ya mdhamini, hapo hapo wamevaa viatu vyekundu!! ni mbumbumbu hadi seems hata shule walipata X kibao kwa kalamu ya mwalimu!
    wanawayumbisha wadhamini na kuingia ghalama ya kuprint logo ingine isiyo yao kiufundi, hata Vodafone wakiona hii hali MD u matatani! kwa nini tumuadhibu kampuni iliyoleta neema kwa ujinga wa yanga? ndio maana yanakuwa ya mwisho kwani uongozi wa hawa ni masubuni matupu! bado tupo mbali sana.
    nawasifu sana simba, seems ni team ya kistarabu. kilimanjaro ni wadhamini wa hizo team mbili, logo ya kili ina njano, ila Simba wanavaa na wanasonga mbele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...