TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE,INAELEZA KWAMBA BASI LA DELUXE (PICHANI) LINALOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA DODOMA NA DAR ES SALAAM,LIMETEKETEA KWA MOTO MAENEO YA KIBAHA KWA MATIUS MKOANI PWANI MARA BAADA YA KUPASUKA KWA TAIRI LA MBELE NA KUPELEKEA KUPASUKA KWA TENKI LA MAFUTA NA KUFANYA MLIPUKO.
AJALI HIYO IMETOKEA NUSU SAA ILIYOPITA KWA MUJIBU WA RIPOTA WETU ALIOPO ENEO LA TUKIO HIVI.
INASEMEKANA WATU 10 TU NDIO WALIOFANIKIWA KUTOKA KWENYE BASI HILO WAKIWA HAI LAKINI WENGINE WOTE WANASADIKIWA KUTEKETEA NA MOTO HUO.
GLOBU YA JAMII INAENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU TUKIO HILO NA TUTAENDELEA KUTOA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZINATUFIKIA.
mungu wasaidie ndg zetu waliopo ktk jali hiyo
ReplyDeletemungu awalaze mahali pema waliopoteza maisha,na awape afya njema walionusurika
ReplyDeleteIts very bad,,alafu serikali inatangaza eti ni watu kumki tu wamepona,,si kweli
ReplyDeleteInasikitisha sana kwani hata waliokufa ni vigumu kuwatambua sura zao kwani miili yao imeharibika vibaya kwa kuungua na moto,,na sura zao hazitambuliki
kikubwa ni tairi ya mbele kuw akipara,,na ain ay abasi yenyewe almaarufu kama UTONG haya ya kichina
kwani mara bada ya mwereka (ups and down) lilibonyea paa,likashukua hivyo kupelekea dimension ya kioo kuwa ndogo hata ya kupitisha kichwa kwa ajili ya kujiokoa ( Haya mabasi bure kabisa) japo yanasifika kwamba hayana mabati ya kujeruhi watu lakini isue ni kwenye moto,,yamkini moto usingewaka wale ndugu zetu wangetoka wote
Mimi kama niliyeshuhudia kw ambali bila kuw ana uwezo w akutoa mdaada wowote kwani moto ulikuw ani mkali mno,,hakuna aliyethubutu kusogelea imenisikitikitisha sana
Ila kikubwa ni tairi ya mbele kuwa kipara na mwendo kasi n agari lililokuw ambele
Ni hayo tu wadau wenzangu
Mdau safarini kutoka Upareni
Imefika wakati Wakubwa walio madarakani hasa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikafikiria kuwa na vituo vya zimamoto katika kila kitongoji hapa jijini na nje ya jiji. Hii ni kwa sababu mji umepanuka sana na wote tunategemea zimamoto itoke FIRE pale eneo la Jangwani Sekondari. Je hii ni haki kweli???
ReplyDeleteMajanga yanaepukika na nadhani hata hapo Kibaha pia wanategemea magari yatoke Dar je hi halali?? Tupende maendeleo na tujiwekee mazingira ambayo yatatusaidia katika shida kama hii ya moto.
Pole ndugu zetu mliopotelewa na ndugu katika ajali hii. Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi. Na kwa walio hospitali tunawaombea wapone haraka.