Mwandishi wa Habari Mwandamizi , Amina Said (ITV) ,akitumbukiza kura yake kwenye sanduku la Mgombea wa Mwen yekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro (MORO PC) wakati wa uchaguzi
Mwandishi wa Habari Mwandamizi , Kasilda Mlimila Mgeni ( STAR TV) ,akitumbukiza kura yake kwenye sanduku la Mgombea wa Mwen yekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro (MORO PC) wakati wa uchaguzi
Mwandishi wa Habari Mwandamizi na Mkongwe wa lililokuwa Shirika la Habari Tanzania ( SHIHATA ), Aidan Libenanga ,akitumbukiza kura yake kwenye sanduku la Mgombea wa Mwen yekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Morogoro (MORO PC) wakati wa uchaguzi uliofanyika
Mwenyekiti mpya wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Morogoro, Aziz Msuya ( wapili kutoka kushoto) akitoa nasaha pamoja na shukrani kwa wajumbe kwa kumchangua yenye na Kamati nzima ili kuiongoza Klabu hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Mlezi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Morogoro (MORO PC) Stephen Mashishanga , ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Mikoa mbalimbali ukiwemo wa Morogoro akitoa nasaha kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo
Baadhi ya Wajumbe wa Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Morogoro ( MORO PC) wakitafakari kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya Uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo ambao ulifanyika |
John Nditi, Morogoro
WANACHAMA wa klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro(MOROPC) Wamewachagua viongozi wapya wa ngazi mbalimbaliwatakaongoza kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Uchaguzi huo ulifanyika Oktoba 22, mwaka huu katika ukumbi wa chama cha Msalaba mwekundu wanachama walimchagua Aziz Msuya kwa kura 32 kuwa mwenyekiti mpya kuchukua nafasi ya Boniventure Mtalimbo ambaye hakugombea nafasi hiyo.
Msuya ambaye ni mwakilishi wa kampuni ya bussnes times alimshinda mpinzani wake Idda Mushi ( ITV) aliyepata kura 25 ,kabla ya hapo Mushi alikuwa makamo mwenyekiti katika uongozi uliopita wakati nafasi ya makamo mwenyekiti ilinyakuliwa na Devota Minja(ITV) baada kupata kura 38 dhidi ya mpinzani wake Ramadhani Libenanga ( Majira) aliyepata kura 16.
Katika nafasi ya katibu ilichukuliwa na Abed Dogoli (ATV) aliyepata kura 44 na kumshinda mpinzani wake Joseph Malembeka (Tanzania Daima ) aliyepata kura 11 ambapo nafasi ya Mweka hazina ilichukuliwa na Samuel Msuya kwa kupigiwa kura za ndio 47 kati ya kura 57 huku nafasi ya mweka hazina msaidizi ilichukuliwa na lilian Lucas (Mwananchi) baada ya kupata kura 30 dhidi ya mpinzani wake Ashton Balaigwa,( Nipashe) aliyepata kura 22.
Kwa upande wa wajumbe wanachama waliwachagua Monica Liampawe(TBC) kwa kura 37 ,latifa Ganzel (UHURU) kura 33 na Venance George (Mwananchi) aliyepata kura 32 ambapo jumla ya wagombea saba walijitokeza kuwania nafasi hizo tatu.
Akizungumza baada ya uchaguzi huo mwenyekiti mpya Aziz Msuya aliwapongeza wajumbe kwa kumchagua na kuhaidi ushirikiano ili kuindeleza klabu hiyo na kuwataka kuacha makundi kwakuwa uchaguzi huo tayari umeshafanyika na viongozi wamepatikana .
Naye Mwandishi mkongwe,Aidan libenanga,aliwataka viongozi hao kuacha tofauti zao za kielimu,au kimaisha na kuheshimu umoja ,ushirikiano na ubunifu ili kuendeleza klabu hiyo ambayo imekuwa mfano kwa klabu nyingine nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...