Dereva wa gari namba T582 AJF aina ya Fuso lililopata ajali septemba 24 mwaka huu na kuua watu 14 na majeruhi 43 (aliyelala )akisomewa mashitaka 44 na Wakili wa Serikali Bw.Griffin mwakapeje, hayupo pichani (Picha na habari na Esther Macha).


DEREVA aliyesababisha vifo vya watu 14 katika ajali iliyotokea eneo la Msangamwelu Wilayani Chunya Bw. Moses Kapus (55)amesomewa mashitaka 44 akiwa chini ya ulinzi katika hospitali ya Rufaa Mbeya .


Ajali hiyo ilitokea septemba 24 mwaka huu majira ya saa 1 .00 usiku baada ya roli aina ya fuso lililokuwa likitokea mnadani eneo la Mbuyuni wilayani Chunya kushindwa kupanda mlima na kuanguka.


Akimsomea mashtaka hayo mbele hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wa Wilaya Bw. Michael Mteite Wakili wa Serikali Bw.Griffin Mwakapeje alidai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na makosa 44.


Bw. Mwakapeje alidai kuwa mshtakiwa Kapus akiwa kama dereva alisababisha ajali kwa uzembe kutokana na kuendesha kwa kasi na kusababisha vifo vya watu 14.


Wakili huyo alidai kuwa dereva huyo akiwa na gari aina ya fuso zenye namba T582 AJF aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na kusababisha majeruhi 43 ambao mpaka sasa hali zao hazijaweza kuwa nzuri na kwamba mshtakiwa huyo alitumia gari hilo kinyume na aliyopewa .


Kwa upande wake Hakimu wa Mahakama hiyo Bw.Mteite alisema mahakama imepokea makosa yote alisomewa mshitakiwa 44.


Hata hivyo mshitakiwa aliomba mahakama impe dhamana kutokana na hali yake kuwa mbaya kiafya, ambapo hata hivyo wakili wa serikali alimwomba Hakimu wa mahakama kuwa masharti ya dhamana yaangaliwe kwanza nay awe magumu kutokana na hali za majeruhi kuwa mbaya.Aidha Hakimu huyo alimtaka mshitakiwa kuwa na fedha taslimu sh. Mil.5 na wadhamini wawili wenye nyumba ili aweze kupata dhamana.


Hata hivyo Wakili wa serikali alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuwa tarehe ya shauri hilo itakuwa Octobar mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mama afande ataki mchezo kazi kweli kweli ukiwa upande wake wa kujidai utakoma

    ReplyDelete
  2. mie nashangaaaa na nadhani ningekuwa mie ndio huyo afande katika picha hii kwanza ningeona hata aibu kusimama katika picha hii. suala la gari za mizigo aina ya fuso na mengineyo kubeba abiria siku za mnada yalishapigwa marufuku na serikali. nadhani wadau mtakumbuka siku chache zilizopita ajali kama hii ilitokea na serikali ilitoa tamko . sasa unakuata ajali kama hii inatokea halafu polisi wa eneo au mkoa husika bila hata aibu wanasema eti 'AJALI HII ILISABABISHWA NA MWENDO WA KASI NA DEREVA ALIKUWA AMEBEBA ABIRIA WAKITOKA AU KUELEKEA MNADANI'... sasa hivi wewe polisi jukumu lako ni nini? wakati huyo jamaaa anapita mwendo kasi mlikuwa wapi? mliruhusuje huyo dereva apite eneo hilo (kwasababu lazima huyo dereva na gari lake wanapita barabarani ambapo kama sio wazee wa tigo fasta wapo basi traffic polisi alikuwepo) wakati tamko lilishatoka kuzuia hilo. mngetakiwa mjiuzulu kwa uzembe huo wakati mnamshitaki huyo muhusika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...