Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande (kushoto), akimwapisha Rais wa Zanzibar na Serikali ya Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Tanzania,Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muundano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete akipena mkono na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein leo mara baada ya Dkt. Shein kula kiapo cha kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Tanzania, Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muundano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Kikwete akiwa katika Mazungumzo na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein,Waziri Mkuu,Mizengo P. Pinda pamoja na Jaji Mkuu,Othman Chande.
Jaji Mkuu wa Tanzania,Othman Chande akibadilishana mawazo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema.
picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nafasi hii inatambulika na kifungu gani cha katiba wadau? Msaada tafadhali.

    ReplyDelete
  2. Hivi Mwakyembe na Mwandosya wanaendeleaje? Serikali, mnaweza kutupatia taarifa za hali za hawa viongozi wetu?

    ReplyDelete
  3. Hiki kitendawili cha huu muungano anaeweza kutuba jibu lake ni Mwalimu na Karume. Too bad hawapo nasi tena. Tutabakia kujiuliza maswali mengi kuhusu huu muungano bila kupata majibu.

    I don't know why Zenjibar bado wanakubali kuwa kwenye huu muungano.

    Jiwe.

    Michu, usibanie hii.

    ReplyDelete
  4. Kutambulika na kifungu cha katiba sio muhim sana ktk nafasi hii !..Kwa vile hana wizara anayoiongoza wala mshahara anaolipwa..Acheni uchochezi, tujadilini mambo ya maendeleo.

    ReplyDelete
  5. Kama alivyouliza mdau juu kifungu gani cha katiba kimetumika? Kwanini anaapishwa sasa wakati baraza la mawaziri limeundwa 2010 mwaka mzima yeye alikuwa wapi?

    ReplyDelete
  6. soma Article 54(1)of the Constitution

    ReplyDelete
  7. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu 54 Ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

    ReplyDelete
  8. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kifungu 54 Ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote.

    ReplyDelete
  9. Kama kifungu 54 Ibara ya kwanza ambayo inawataja wajumbe wa Baraza la Mawaziri kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Mawaziri wote. KWANINI ANAAPISHWA LEO 10/24/2011?? BARAZA LIPO TAYARI ZAIDI YA MWAKA NA NUSU. INA MAANA ALIKUWA HAUDHURII VIKAO VILIVYOPITA?? KWANINI KAMA KATIBA INASEMA ANATAKAIWA AWEPO KWENYE VIKAO??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...