Na John Kitime
Jambo ambalo naliona wazi ni kuwa Watanzania wanapenda sana nyimbo za dansi zinazotokana na nyimbo zenye asili ya makabila ya hapa Tanzania. Nikikumbuka nyimbo kama Mtaulage, Malaine, Nyongise, ambazo ni kazi yangu mwenyewe nikiwa Tancut na Vijana Jazz, kila Munu ave na kwao ya Les Mwenge, Boko wa Kilimanjaro Band, Shakaza ya Bantu na nyingi nyingine zote zilichukua nafasi ya juu katika anga za muziki wakati wake, na hata sasa.
Pengine lingekuwa somo kwa wanamuziki wa Tanzania na kuliangalia hili katika tungo zao. Hebu tumkumbuke Eddy Sheggy hapa akiwa na Bantu, akiimba na ndugu zaki Francis na Christian.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...