Fainali za kuwania taji la Miss Utalii Tanzania 2011/12 zimeanza kupamba moto, katika ngazi mbalimbali ikiwemo ngazi za Mikoa ambapo hivi karibuni mkoa wa Mara ulipata mshindi wa Taji la Miss Utalii Mara 2011/12 katika fainali zilizo fanyika katika ukumbi wa Bwalo la Magereza Musoma,na kushirikisha jumla ya warembo 12. Katika fainali hizo ambazo zilitumbuizwa na wanamuziki nguli wa THT Lina Sanga na  Ditto.

Mrembo Gaudensia Joseph (pichani juu kati) kutoka wilaya ya Musoma mjini akiwabwaga wenzie 11 na kutwaa taji hilo la Miss Utalii Mara 2011/12. Mshindi wa pili alikuwa ni Suzan Mathias (shoto) kutoka Wilaya ya Bunda na mshindi wa Tatu alikuwa ni Doreen Charles (kulia) kutoka wilaya ya Tarime.

Katika shindano hilo ambalo lilihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Mara na maeneo ya jirani,mshindi alizawadiwa sh.1,000,000/=,wa pili Sh 800,000/= na wa tatu sh 500,000/= huku walio bali wakipewa kila mmoja sh 100,000/=
Washiriki wa Miss Utalii mkoa wa Mara wakiwa jukwaani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. uncle hivi unafanya utani? yaani huyo binti ndie alieshinda kweli? sisemi mengi ukaja ukaniweka pakachani lakini !?!!!!

    ReplyDelete
  2. Mmh.....are they serious?!

    ReplyDelete
  3. Oyaa, uzuri unategemea na sehemu pamoja na washindani wenyewe, mwisho wa siku ni lazima apatikane miss na sio kuahirisha!

    Hata hivyo, mbona huyu dada ni mzuri sana, sura yake ndefu ndefu na macho angaza, pua mshale na kidevu cha samaki, au hamna macho?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...