Ndugu Issa Michuzi,
nakupongeza sana kwa kazi nzuri ya kutupatia habari mbali mabali.
Mimi ninamoja tu la kuchangia kuhusu ndugu Lowassa kujitokeza.....kwa vyombo vya habari.

Amefanya vyema sana..katika ulimwengu huu wa free media kueleza ukweli wa mambo..mbali na hilo '..... mimi ninapendekezo langu kwa ndugu Mheshimiwa Lowassa
arejee kwenye ulingo wa siasa kwani ukichukua mizani na kupima viongozi tulionao hivi sasa ni yeye pekee anasimama... ukizingatia yafuatayo
-Uwajibikaji......

-Kusimamia sheria na haki..
-Lowassa ni mtendaji na mchapa kazi..
-Ni Lowassa aliena-uwezo wa ku-discipline watendaji wake katika sekta mbali mbali hasa vyombo vya umma...
-He is innovative..politically and economically si mdesaji....
-Katika hali mbaya ya uchumi tulionao hivi sasa he can focus ahead..tuna tatizo hilo hivi sasa..

viongozi bado wanafikiri kuwa hali tulionayo hivi sasa itaendelea..look the otherway kila utakaye zungumza naye hivi sasa kutoka tanzania anakwambia mambo ni mazuri....hili ni tatizo la vision.

Asante sana ndugu michuzi kama uta-post maoni yangu...
--vigumu vyama vya siasa.....muda wa siasa umepita lets look into the economy..Je watoto wetu tutawaachia nini...

Thanks
Mzalendo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. We mdau una ajenda yako binafsi na inaelekea unaishi katika ulimwengu danganyifu na wa kifisadi, uko gizani na wala hujitambui ungali kizani. Pole sana!

    ReplyDelete
  2. huu wote ni upuzi mtupu, yawezakana huyu ni sehemu yake.kuna Wtz wenye vision ya kweli na nia ya kweli zaidi ya Lowasa.Huyu ndie katufikasha hapa tulipo sasa na mikatabaka ya Richmond, Dowans na mengineo kama hayo na KARAMAGI pale tics na Rostam kwa Kampuni ya Caspian mining ltd na mengine mengi tu.

    ReplyDelete
  3. WEWE NI WALE WALE!!!USITUCHEFUE SAA HIZI NYIE NDIO MNAOTUMWA KWENYE MAANDAMANO BILA KUPIMA NI KWA FAIDA YA NANI MNAENDA. NYERERE ALIWAITA MAZUZU

    ReplyDelete
  4. Wewe mtoa mada umedumaa kifikra unafikiri ni baadhi ya watu tu wanazeza kufanya mabadiliko. Una mawazo ya kikabwela na uko tayari kuongozwa na wazee hadi mwisho wa maisha yako. We si mtu wa mabadiliko. Wewe ungeambiwa Obama angeweza kuwa raisi usingeamini sababu unafikra kwamba ni watu wa aina fulani tu wanaweza kufanya mambo mazuri. Tanzania in watu takribani 4o millioni sasa. Je, ni kweli kwamba ni mchapakazi mmoja aliwekwishajilimbikizia mali ndio anaweza kutukomboa? WAKE UP! Kwa maoni yangu waziri mkuu wa sasa anaguswa na hali ya watu wa chini kuliko huyo unayemtetea. Kama unapenda kuinua hali ya wengine kwa nini unajilimbikizia wewe tu na kuwasahau hao unaowatumikia?

    ReplyDelete
  5. well said mzalendo...though its hard kwa watu wenye upeo mfupi kuelewa hilo... Anonymous one wewe ndio hujitambui coz ur speaking without evidence tupe kielelezo yakinifu ambacho ni beyond reasonable doubt kinachofanya uhusishe what he said na ufusadi na ufisadi huo ni wanani...please watu tuache maneno ya barabarani na tuwe na data kamili before kumhusisha mtu yoyote na alegation ambazo hatuna uhakika nazo

    ReplyDelete
  6. Pamoja na hayo yote, tunachojua next president lazima atoke upande wa pili wa Muungano, nadhani ni busara na ni msukumo katika maendeleo, hao wajiandae kwa Umakamu.

    ReplyDelete
  7. Ah tatizo lenu watanzania ndio hili la ubishi ambao hauna vision yoyote,ni kweli anayosema mtoa mada hii kuwa tunaambia mambo mazuri bongo,home sweet home.

    lakini ukishuka tu bongo tz utaona walala hoi kibao,vijana wadogo wanauza njugu,wengine usiku wanalala njee,mchana unawaona wanasukuma warikwama,maisha gani hayaya mtanzania ?

    Vijana wanachoakata wakati huu ni ajira,elimu,serikali ijikite sana katika elimu,iwaharamie vijana wake,iwe japo elimu ya ufundi,tatizo vijana wanashindwa kuingia katika elimu kutokana hawana uwezo wa ku afford accomodation na chakula,huduma ya afya.

    Nchi zilizo endelea zinawalipia huduma hizo zote kutoka kwa serikali ,vijana wanapata elimu japo ya kutia tize au capnter ili aweze kupa opportunitis za ajira.

    Serikali wakati huu umejikita sana katika siasa tukisoma siku zote magazeti tunaona madogo tu ya ksiasa jamani wakati huu tunataka kuona taifa lina songa mbele,kwa pando zote,kiuchumi na kijamii.

    Sorry wazalendo.

    ReplyDelete
  8. Mi nashangaa ni Lowasa tu ameonekana mfisadi? Mbona karibia wote wameoza? kila siku lowasa, hamuwathubutu hao wengine. Au kwakuwa Wtz ni waoga kusema ukweli.? naomba michu usinibanie pls maana siku hizi nawe

    ReplyDelete
  9. watanzania tuende na wakati,kuna vijana wengi wasomi ambao wanaweza kuleta mambo mapya kwenye serikali,lakini sisi bado tunawapigia debe wazee walioza debe what for?tunataka madiliko, ndiyo maana kuna kuzaliwa pia kuna kufa acha porojo zako wewe unamtetea mfisadi mkubwa kama lowasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...