Dear Blog ya Jamii,


Naomba CRDB Bank waweke wazi tatizo la mara kwa mara kwenye ATM zao kwani sisi wateja tunapata usumbufu na gharama za ziada kwa ajili ya ATM kuzimika haswa mida ya 06:00-0700. Wateja tunaitaji kuambiwa ukweli na uwazi

Mdau mpingarushwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Huo huwa ni muda wa kujaza upya hela baada ya kuwa zimeshachukuliwa mchana kutwa

    ReplyDelete
  2. Kwakweli inakera. nakichokera zaidi imekuwa kama ratiba yao sas. Wakati wa jioni kuanza saa 11 paka saa moja usiku hali hio pia hujitokeza. Inaudhi na kukera. Wajirekebishe

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu unayedai kwamba huo ni muda wa kujaza hela, nahisi utakuwa unafanya kazi CRDB. Kwani lazima ATM zote zijazwe hela wakati mmoja? Hata mimi ninapata shida sana na muda huu. Kama ni kweli, basi watuandikie tangazo katika ATM kwamba muda huo utakuwa reserved kwa ajili ya kujaza hela

    ReplyDelete
  4. Reputation ya CRDB imeanza kushuka nafikiri hawana risk manager mzuri, lakini angekuwepo angejua kwamba the moment ATM haina hela ana suffer a very high level reputation risk ambapo in just a week tyme unaweza kuta deposits zinashuka vibaya and you loose customers, au kwakuwa wana enjoy sort of a monopoly! lakini one day they will know kwamba they are doing bad, mimi nimewahi pata shida sana cku moja halaf nilikuwa nimepata mgeni wa kimataifa akanishangaa sana ikabidi kesho yake nifungue akaunt Barclays, and infact some of my money ziko huko. Dr. Kimei we respect you, do something urgently!
    Mdau

    ReplyDelete
  5. Naona hapo vilevile kuna tatizo la lugha gongana " Is closed for Maintenance service" Hapo mwandishi atufafanulie nini maana ya maintenance na nini maana ya service kwa mtazamo wangu ni msamiati rudio! Kwanini isingetumika lugha ya kiswahili " ATM haitumiki kwa sasa kwaajili ya matatizo ya kiufundi, huduma itarudishwa mara matengenezo yatakapokamilika samahani kwa usumbufu. Ilipaswa zitumike lugha mbili ya kiinglishi na kiswahili hapo! au mnasemaje wadau?

    ReplyDelete
  6. Alafu ankal hii ni message yako, unatakiwa kupasha moto blog yetu, leta topic ya usumbufu tuigombanie kwani ni siku nyingi haujaleta usumbufu kwa kwenye blog, tunataka chemsha bongo umekuwa too nice kwa muda mrefu. Tunga kitu chochote controversial! hahahahaaaaa

    ReplyDelete
  7. atm zote za crdb zinakuwa off line kuanzia saa 12 hadi saa moja usiku kutokana na systeam inayotumika na bank mda huo head office wanacollect transaction za all atm in tanzania na kubalanzisha ni tataizo la kimfumo tu na wala si kuishiwa na hela tuvumilieni mpaka tutakapopata system bora zaidi

    ReplyDelete
  8. "Anonymous Sat Oct 08, 05:13:00" AM 2011 ATM is closed for maintenance ni sentensi inayojitegemea na service will be restored soon ni sentensi nyingine please!!!.

    Haya yote ndio globalization si tunaelekea kuwa kijiji? Hela ni yako na bado unapangiwa muda wa kuipata ikimaanisha pia unapangiwa muda kuitumia. Kama mifumo hiyo ya kigeni haifanyi kazi na wewe unatakiwa usubiri...modernization ktk speed ya kinyonga asiyewinda!!

    CRDB you still have a good reputation but do not play with it coz though you are said to have monopoly competition may take you back to square one in a blink of an eye!!

    CRDB customer forever!

    ReplyDelete
  9. Hapa tumeshawajua wafanyakazi wa CRDB ni akina nani. Globu ya Jamii oyeeee!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...