Katibu wa NEC, Oganaizesheni Asha Abdallah Juma (katikati) akishangilia pamoja na wana-CCM wengine katika hoteli ya The Peak mjini Igunga baada ya kupata matokeo ya awali usiku wa kuamkia leo.
 Mkurugenzi wa Tanzania One Theatre (TOT) John Komba aking'ang'aniwa kwa furaha na watu waliopata matokeo ya awali kuwa CCM imeshinda.
 Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama na Katibu wa NEC Uchumi, Fedha, Mwigulu Nchemba na baadhi ya watu waliokuwa katika hoteli ya The Peak mjini Igunga wakishangilia usiku wakuamkia leo, baada ya kupata matokeo ya awali kutoka kwenye vituo kwamba CCM inaongoza



 Juu  na chini  jopo la wataalam wa CCM wakijumlisha matokeo usiku wa kuamkia leo, kutoka kwa mawakala wa CCM kutoka vituo mbalimbali baada ya uchaguzi mdogo jimbo la Igunga kumalizika. Hadi sasa matokeo yanaonyesha kwamba CCM inaongoza kwa zaidi ya kura 4000. Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu ili kupata matokeo rasmi..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. hii ndio nchi ccm oyeeeeeeeeeeeee hakuna wa kuwafananisha na nyie hongera sana kabineti nzima ya ccm bila kumsahau raisi wetu mstaafu mh ben mkapa kwa juhudi zake alizo zionyesha huko igunga hongera sana mzee bado tunakupenda

    ReplyDelete
  2. TUPONGEZANE WANA CCM NI KAZI NZURI NA HASA BAADA YA KUWA NA USHIRIKIANO TANGU MWANZO KWA KWELI IMELETA RAHA SANA SASA KAZI NI MOJA KILA UNAPOTOKEA UCHAGUZI MSHIKAMANO NI HUO HUO NA MIKUTANO YA MARA KWA MARA NA WANANCHI ILI KUJUA MATATIZO YAO NA KURATIBU MAENDELEO NA KUFUATILIA MAAGIZO YA CHAMA KTK MIRADI NA SERA ZA CCM KWA PAMOJA HIYO ITATUFANYA KUWA KARIBU NA WANANCHI KIKAMILIFU NA KUTOTOA MIANYA YA WAPINZANI KUTUMBUKIZA FITINA ZAO ZA UZANDIKI KWA WANANCHI TUNAONA WANAIGUNGA WAMEONA PUMBA NA MCHELE NA WAMECHAGUA KILICHO BORA KABISA CCM OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE KWA KWENDA MBELE mdau richie wa ughaibuni

    ReplyDelete
  3. Wewe ulieandika maoni hapo juu na kuishangilia CCM imekufanya nn? kwanza fikiri Igunga ina barabara moja ya lami tu, Zilizobaki ni za vumbi. miaka mingapi? CCM imekaa bungeni nadhani CCM wamepata kura za watu wa kutoka vijiji wasiojua nn maana ya maisha. Ila mapambano bado yataendelea tu na CHADEMA itachukua nchi achana na hao wa vijijini hawajasoma sikuhizi wasomi wengi vijana na CHADEMA ni vijana kazi ni kwanu tunawasubiri kwa hamu 2015, kama Rais mwenyewe alkiri kuna mapambano ya uhakika mwaka 2015,CHADEMA OYE KUWENI WAZI TANGAZENI MATOKEO NINI KUJISUASUA MAFISADI WAKUBWA CCM,

    ReplyDelete
  4. Hivi chama kilicho kuwa na mgombea ni kimoja tu, mbona Blog haituambii kuhusu wapinzani wa siasa ya Tanzania walikuwaje usiku wa kuamkia lea ktk uchaguzi,ukitaka chombo chako cha habari kipendwa kisiwe na upendeleo. Ok flocks.

    ReplyDelete
  5. Biashara ya maneno na vibweka na iishe sasa kila mmoja arudi kusukuma gurudumu la maendeleo. Tumepoteza nguvu kazi nyingi mno pale igunga na ninatumaini sasa zitaanza kesi ili tuendelee kupiga domo, ohoo, tumeibiwa, wamechakachua nk..
    Kwa kiingereza cha kenya tuseme sasa na tu "NGO MBACK 2 WAK".

    ReplyDelete
  6. Igunga ina barabara moja tu ya lami?
    Kawaulize wanaigunga mahitaji yao, mambo ya kudhani maendeleo ni lami naona si kuwatendea haki wananchi na ni siasa makengeza. Afadhali ungeongea juu ya maji kwa matumizi yao na mang'ombe yao labda ningeona busara

    ReplyDelete
  7. Hayo maneno ya kashfa kuwa watu wa vjjin hawajasoma, hawajui maisha ndiyo yaliyofanya wawapige chini.Na haya mambo ya imewafanyia nini ndiyo chambo kwani na wewe umeifanyia nini. Unajua angalau maana ya MKURABITA au unataka kufanyiwa tu, acha hizo dogo kuwa mstaarabu hizi shamra shamra za kurundika mafanikio ya miaka 50 ya uhuru ni ya ccm kwa kweli (japo hupendi). Vua hiyo miwani ya mbao.

    ReplyDelete
  8. kaka michuzi kama unashabikia ccm vile hahahaha kwa lipi kaka au na ww upo kwenye kutafuna shamba lala bibi...kawaida yako kubana comment zangu ila najua ujumbe umefika
    MDAU NORWAY

    ReplyDelete
  9. Yaani kizazi cha dtcm kinajumlisha matokeo kwa peni??????????????

    ReplyDelete
  10. Hapo mmepata,Ila oneni sisi wakazi wa ARUSHA jinsi majimbo yetu yalivyotawaliwa na CHADEMA tunajua nn wanachokifanya hata kwenye buge CCM wenyewe wanaaibishana, Hata spika wa buge aliepita alisema ndani ya nchi kuna mawaziri sita kama jina lake Ex.Mbuge wa same huyo tunampa bigup mama, waliobakia wote wanalisukuma bunge na wana CCM WAO CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE * 100

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...