Bendera ya Umoja wa Mataifa (UN) ikipandishwa juu, ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 66 ya Siku ya Umoja wa Mataifa. Wizara ya Mambo ya Nje imeshirikiana na UN katika maonesho yake ya Wiki ya Wizara, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Mhe. Waziri Benard K. Membe akikagua gwaride la heshima, kabla ya bendera ya Umoja wa Mataifa kupandishwa rasmi ikiwa ni ishara ya maadhimisho ya miaka 66 ya Siku ya Umoja wa Kimataifa (UN Day).
Mhe. Waziri Bernard K. Membe akisalimiana na baadhi ya wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa (UN), baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Umoja wa Mataifa unasheherekea miaka 66 tangu kuanzishwa kwake, ambapo Mhe. Waziri alisema changamoto moja iliyopo sasa ni ya kuzishirikisha nchi za Afrika ili kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili bara la Afrika. Alitoa mfano mmoja wa nchi ya Somalia, ambayo ina watu zaidi ya milioni 3 wanaokufa na njaa, na kwamba Umoja huo una jukumu la kutoa misaada ili kusaidia migogoro inayozikabili nchi za Afrika.
Mhe. Waziri Membe akihutubia katika maadhimisho ya miaka 66 ya Siku ya Umoja wa Mataifa (UN Day) na kilele cha maonesho ya Wiki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya hotuba yake, Mhe. Membe alisema Tanzania ina namna nyingi za kujivunia amani na aliwasihi vijana wasiige yale yaliyotokea nchini Libya. "Tujisifu kuwa, Tanzania ilikuwa na kiongozi shupavu hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alikataa ukoloni au mauaji ya aina yoyote na ambaye alijenga msingi wa usawa kwa binadamu wote," alisema. Sifa hizo zimeifanya Tanzania itambulike na iheshimike duniani kote.
Mabalozi wastaafu wakiwemo Mhe. Balozi John Rupia na Mhe. Mustapha Nyang'anyi, wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri Membe wakati wa kilele cha maonesho ya Wiki ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikiwa ni sehemu za maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na sherehe za miaka 66 ya Siku ya Dunia ya Umoja wa Mataifa. Maonesho hayo yalifanyika kuanzia tarehe 21 hadi 24 Oktoba kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Nawaona wastaafu wamempumzika, balozi nyanganyi tunakumiss huku Washington! Ule umoja wa watanzania uliouimarisha kwishnet hakuna tena! Hakuna picknick za umoja wala nini. Tunakutana kwenye misiba, harusi, baby shower na mengineyo. Hakuna shughuli ya jumuiya ya watanzania tena hapa DMV!
ReplyDelete