MPENDWA MAMA YETU JOYCE PETER NKURLU, ILIKUWA SIKU, MWEZI NA HATIMAYE MIAKA MIWILI SASA TANGU UTUTOKE TAREHE 12/10/2009 KATIKA DUNIA HII.

 LAKINI TUNAFARIJIKA KWA SABABU TUNA AMANI UKO PAMOJA NASI KIROHO SIKU ZOTE.

MAMA HAKUNA SIKU IPITAYO KWETU BILA KUKUMBUKA KWA UPENDO, UKARIMU NA KUJALI KWAKO KATIKA KUTULEA NA KUTUUNGANISHA SISI WANAO NA FAMILIA PAMOJA. HAKIKA UPENDO WAKO UMEKUWA DIRA NA NURU KATIKA MAISHA YETU.TUNAENDELEA KUKUOMBEA NA TUNAENDELEZA YALIYO MEMA KWA WAJUKUU ZAKO UPUMZIKE KWA AMANI.

DAIMA UNAKUMBUKWA NA WATOTO WAKO: ATUZA, ANGAZA, AMANI, NZIGIA, MATINA NA MASALA. 

WAJUKUU ZAKO AMANI, VANESSA-SALOME NA NGULLA, BILA KUSAHAU MAMA YAKO, DADA NA KAKA ZAKO WOTE, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI PAMOJA NA WAUMINI WENZAKO. DAIMA TUTAKUKUMBUKA MILELE.

MAMA TULIKUPENDA SANA, LAKINI MUNGU BABA WA MBINGUNI ALIKUPENDA ZAIDI.BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. ANKAL TUNAKUSHUKURU SANA KWA KUTUPATIA TAARIFA KILA SIKU BILA KUCHOKA. INGEKUWA NI BUSARA KAMA UTAWATAKA RADHI WADAU KUTOKANA NA TAARIFA ISIYO YA KWELI KUWA MWAKIMU ALING'ATUKA MWAKA 1985. NAFIKIRI ALIJIUZURU URAIS MWAKA 1985 NA KUNG'ATUKA UWENYEKITI WA CCM MWAKA 1987. KUREKEBISHA NA KUOMBA RADHI NI KITU CHA KAWAIDA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...