![]() |
Siku ya kumeremeta kwa Juliana Njohole na William Lyapembile miaka 52 iliyopita |
Maharusi na wapambe wao katika sherehe yao majuzi
Mwaka 1959, October 8 wazazi wetu walifunga ndoa katika kijiji cha Mngeta, Kilombero - Morogoro kama inavyoonekana kwenye hiyo picha ya black and white. Mwaka huu wametimiza miaka 52 ya ndoa, misa ya shukrani na sherehe za kuwapongeza zilifanyika kijijini Mngeta, kwenye kanisa lile lile walilofunga ndoa miaka 52 iliyopita.
Liliowavutia watu wengi ni wale flower girls watano walikuwa wakitupa maua na kushikilia shela ya bibi harusi miaka 52 iliyopita, Kwa bahati wote wako hai na wakaifanya kazi yao ile ile walioifanya miaka 52 iliyopita. Hao wakina mama waliowazunguka maharusi, ndio vibinti vilivyoshika shela kwenye hiyo picha ya black and white. Mwaka 1952 mabinti hao walikuwa na miaka 8 tu. Leo hii wote ni wastaafu lakini walihakikisha wanawasimamia tena maharusi wao.
Mama anaitwa Julliana Njohole ametimiza miaka 76 tarehe 4 October mwaka huu, na baba William Lyapembile atatimiza miaka 80 tarehe 31 December mwaka huu.
Wasimamizi (Matron & Best man) ni mjukuu wao wa kwanza kuolewa (Modesta Machengo) akiwa na Mumewe Richard.
Tunawapa pongezi nyingi wazazi wetu kwa kuwa mfano wa ndoa ya kuigwa. Mama alipoulizwa nini siri ya ndoa yao kudumu miaka mingi, alisema ni uvumilivu na kusamehena, na silaha kubwa zaidi ni sala.
Tunawapenda sana wazazi wetu, tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kuwapa afya njema ya mwili na roho.
Kwa mapicha zaidi ya sherehe hii BOFYA HAPA
Kwa mapicha zaidi ya sherehe hii BOFYA HAPA
Aisee hii ni nzuri sana hakika Mungu ni mwema, Hongereni sana baba na mama Lyapembile, Mungu aendelee kuwaopigania mdumu pendoni na msimamie vyema kiapo cha ndoa yenu.
ReplyDeleteMkandawire
WOOOWWWW.....I LOVE THIS....HONGERENI SANA. HUU NI MFANO WA KUIGWA.......SIWAFAHAMU BUT IM SO PROUD OF YOU TWO AND THE WHOLE FAMILY. MAY GOD BLESS YOU.
ReplyDeleteafadhali kuweka positive stories kama hizi kuliko mambo ya kufa kufa na shida shida na skendo skendo
ReplyDeletendo nini hii sasa kweli sisi wabongo masikin ila kwa kutuia pesa kwa mambo ya kianasa tunaweza
ReplyDeleteHongera sana. Mungu Azidi kuwabariki muendelee kuwa kioo kwa wengine.
ReplyDeleteHongereni sana. Michuzi, hizi ziwe picha za mwaka kwa ajili ya kufunza jamii maadili ya ndoa.
ReplyDeleteMungu awazidishie umri afya na furaha
ReplyDeleteWakatabahu
Mimi siyo mpz wa ku comment lakini leo nimeshindwa kujizuia. Hii ni story na picha ya mwaka 2012. Hii ni nzuri sana Mungu azidi kuwabariki na kuwapa maisha mema
ReplyDeleteWewe mdau wa 12:03 wacha wivu. Ni bahati iliyoje kwa wazazi wakawa hai na kusherehekea miaka yao mingi ya ndoa? Mungu haileti bahati hii mara mbili.
ReplyDeleteWatoto na wajukuu kama wanao uwezo na washerehekee tu kwani muda ndiyo unayoyoma. Hongereni sana kwa kuorganise function kama hiyo.
Nawaonea wivu I wish my parents were alive! God bless you.
Nyinyi watoto wa maharusi mlichonifurahisha zaidi hapa ni kwamba taarifa yote hii mmeziandika kwa kiswahili. Ingawa bado tuu watoa maoni wakaja na "WOWWWWW I BLESS THIS GOD...."
ReplyDeleteMungu ashukuriwe na hongera sana wazazi wetu kwa kuonyesha mfano mzuri sana kwa kizazi kipya.
ReplyDeleteda,this is fantastic.many conglats.nawaombea maharusi maisha marefu
ReplyDeleteHONGERENI SANA. MUNGU AWABARIKI. NI WACHACHE SANA WANAOBAHATIKA KUFIKISHA MIAKA 50 YA NDOA. NDOA NYINGI HUVUNJIKA AU MMOJA WA WANANDOA KUFARIKI MAPEMA
ReplyDeleteHongereni maharusi. Mwenyezi Mungu awabariki na kuongeza miaka 20 zaidi.
ReplyDelete