Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst) Salome Suzette Kaganda akiwafariji wafiwa katika Mazishi ya Mtumishi wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi, Marehemu Kedmon Danford Mgatta aliyefariki tarehe 10/10/2011 Mjini Morogoro ambako alikuwa akipatiwa matibabu ikiwa ni siku tano baada ya kuhitimu Mafunzo ya Upelelezi yaliyohitimishwa na Mhe. Rais Jakaya Kikwete katika Chuo cha Polisi Kidatu.
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst) Salome Suzette Kaganda akiwafariji wafiwa
Waombolezaji msibani. Marehemu Kedmon Mgatta aliyeacha Mke na Mtoto mmoja, alizikwa jana katika Kijiji cha Hogoro kilichopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma ambako alizaliwa mnamo tarehe 15/7/1975. Misa ya Mazishi hayo yaliyofanyika katika Kanisa la Anglikan kijijini hapo na ilihudhuriwa na Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst) Salome Suzette Kaganda, Wakuu na Watumishi wa Sekretarieti ya Maadili, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro na Wageni kutoka sehemu mbalimbali.
Kamishna wa Maadili, Jaji (Mst) Salome Suzette Kaganda akiweka shada la maua kaburini baada ya maziko. Picha na maelezo na Kajiru Shaban - Afisa Habari wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Kanda ya Kati.
RIP kaka Kedmon....
ReplyDelete