BONDIA MBWANA MATUMLA ATAMBA KUMUANGUSHA MPINZANI WAKE FRANCIS MIYEYUSHO KTK RAUNDI YA TANO YA MPAMBANO WAO TAKAOFANYIKA DIAMOND JUBILEE HALL TAREHE 30.10.2011.WAKATI MBWANA AKIJITAPA HIVYO MPINZANI WAKE FRANCIS MIYEYUSHO YEYE AMESEMA WASHABIKI HASA WA KINONDONI WAJE KWA WINGI SIKU HIYO KUSHUHUDIA JINSI ATAKAVYOMTANDIKA MATUMLA NA KUMMALIZA RAUNDI YA 8.PAMBANO HILI KALI LA UBINGWA WA MABARA WA UBO LIMEANDALIWA NA KAMPUNI YA DARWORLD LINKS LTD NA LITAKUWA LA RAUNDI 12.AKIZUNGUMZIA ZAIDI MPAMBANO HUO MKURUGENZI WA DARWORLD LINKS LTD MOHAMED BAWAZIR ALISEMA MAANDALIZI YANAENDELEA VIZURI IKIWEMO MPAMBANO WA KINA DADA ASHA NGEDERE NA SALMA KIOBWA NA KUWATAKA WAPENZI WA MCHEZO HUU WAKE KWA WAUME WAJE KWA WINGI SIKU HIYO KUSHUHUDIA AINA TOFAUTI YA UANDAAJI WA MAPAMBANO YA NGUMI INGAWA SUALA LA UDHAMINI LIMEKUWA NI TATIZO SANA KTK UPANDE WA BOXING NA KUYASHUKURU MAKAMPUNI YALIYOTOA SAPOTI MPAKA SASA AMBAYO NI  JB BELMONT HOTEL,GAZETI LA JAMBO LEO,MICHUZI BLOG,GENESIS HEALTH GYM NA KELKEN GYM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...