Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda yuko nchini Uswisi kuhudhuria Mkutano wa 125 wa  Chama cha Muungano wa Mabunge Ulimwenguni (Interparlimentary Union-IPU). Hapa akipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na Uswisi Balozi A. Ngemera mara alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa mkutano jana jioni.
 Balozi Ngemera akimpa Mhe. Spika Anne Makinda muhtasari wa mkutano
 Katibu Mkuu wa Chama cha mabunge ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Parliamentary Association-CPA) Dkt William Shija akimkaribisha mkutanoni  na Spika Anne Makinda.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akihutubia wakati wa ufunguzi wa mkutano wa  125 wa IPU katika mji wa Bern. Hotuba yake iliyowavuta wengi ilihusu changamoto zinazoikabili dunia ya leo: “siyo upungufu wa bajeti bali ni upungufu wa imani kwa serikali na taasisi mbalimbali”.
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Abdirahin Abdi
MHE. David Kafulila akiwa na mbunge rafiki yake kutoka Canada

Kamishna wa Tume ya Huduma za Bunge Mhe. Hamad Rashid na aliyekuwa Mbunge wa Busega Dkt. Chegeni
Muwakilishi wa Katibu wa Bunge la Tanzania Bw. John Joel na katibu wa msafara Bw. James Warburg.
Mtoto akitoa burudani kwenye ufunguzi wa mkutano huo
Spika wa Bunge Mh. Anne Makinda akiongea na  Balozi Ngemera 
Spika wa Bunge Mh. Makinda  na Balozi Ngemera na ujumbe wa Tanzania 
wakiingia ukumbini.
Mh. Spika Anne Makinda na Spika wa Bunge la Uganga Mhe. Rebecca Alitwala Kadaga wakiifuatilia hotuba hiyo kwa umakini mkubwa.
Maspika, Wabunge, Makatibu wa Bunge, Maafisa na watendaji mbalimbali katika mabunge duniani wakifuatilia hotuba za ufunguzi: Dkt. Williama Shija.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban –Ki Moon akipanda jukwaani tayari kwa kutoa hotuba yake.
Ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania: Mhe. Susan Lyimo, Dkt Chegeni (mbunge wa zamani), Mhe. Hamad Rashid na Angela Kairuki.
Picha ya pamoja ya Spika wa Bunge, Balozi Ngemera na ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania
Sehemu ya washiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...