Ankali pole na majukumu ya kila siku katika blogu yetu hii ya jamii, lakini ingefaa iitwe blogu ya jamii ya kimataifa maana unatujuza mambo mengi mazuri. Ankal leo nina hoja kuhusu sisi wakazi wa kigamboni na suala la ulinzi na usalama.

Kama wajuavyo watu wote kuwa serikali imetangaza mradi wa kuboresha mji wa kigamboni kuwa mji wa kisasa na hii imesababisha mji huu kukua kwa kasi kubwa sana hasa maeneo ya kibada, Gezaulole (Geza uone!), Mwongozo na Kisota. Hii inaweza kushuhudiwa na wingi wa watu wanaovuka kila siku na urefu wa foleni za Magari kuingia kwenye kivuko kila siku.

Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, katika maeneo ya Gezaulole Kibada, Mwongozo, Kisota na maeneo mengine na wengi wa wahamiaji ni wageni walionunua viwanja huko kumekua na ongezeko la wizi au uvamizi wa usiku wa manane na makundi ya vijana katika makazi ya watu hasa maeneo hayo niliyoyataja na kuwapora na hata kujeruhi muda mwingine na hii inatokana na kutokuwepo kwa ulinzi mzuri maeneo niliyoyataja, ukiangalia utaona kuwa kuna kituo kimoja kikubwa kilichopo Kigamboni maeneo jirani na hospitali, ambapo zamani ndio watu wengi waliishi huko, kuna kituo kidogo Feri pale kwenye kivuko na kingine kipo Mjimwema, kama kuna vingine maeneo ya tungi wadau watanirekebisha.

Ukitoka Mjimwema mpaka Kongowe au hadi Mwasonga hakuna kituo hata kimoja umbali wa Km kama 18 hivi, hii inawapa mwanya wezi/vibaka na hata majambazi kufanya uhalifu na kukimbia kiurahisi sana kwa mwelekeo wa Kongowe au Kurasini.

Hivyo bila ya kuzungumza saaana , naliomba jeshi la polisi kutuongezea Kituo kikubwa pale Kibada njia panda ya kwenda Kisarawe II na kidogo kiwe pale Mwongozo baada ya daraja katka barabara iendayo kimbiji hii inaweza kupungu kama si kuondoa uhalifu maeneo hayo na kuwafanya wananchi kushiriki shughuli za kukuza uchumi kikamilifu.

Ankal naomba usiiweke hoja hii kapuni, ili wadau wapate kuchangia na huenda tunaweza pata msaada huu toka jeshi la Polisi, tupo tayari kutoa maeneo kwa ajili ya huduma hii.

Mdau Mbegu- Ungindoni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mdau Kibada Kituo cha polisi kimejengwa nazani muda sasa kwa maana ya jengo na eneo ambalo wewe umelipendekeza la njia panda mbele kidogo ya dispensari. Nafikiri polisi watusaidie lini kitaanza kazi?

    ReplyDelete
  2. kwa kweli ndugu yangu umeongea maneno mazuri sana lakini sehemu ulizotaja ningependekeza pia na tuangoma sababu wezi wengi wanaokuja pale sasa hivi wanatoka mbagala na tuangoma imekuwa kwa kiasi kikubwa kwa sasa!Napia tuwalaumu wizara ya Ardhi sbb wao ndio waliotangaza kupanuwa mji na kuahidi hayo yote wangeyaleta pamoja na maji na umeme na mahospitali pia!

    ReplyDelete
  3. Kwani hujui kuwa polisi ndio wezi na majambazi?maana wanashirikiana nao na wanawapa/kuwaazima silaha.
    Unaomba majamvi kwenye shughuli kaka?
    Nunua bastola yako ujilinde mwenyewe hii ndio bongo hakuna wa kumsaidia mwenzake kila mtu kivyake.
    "Tanzania ni kama tunda pori halina mwenyewe",maneno ya mbunge fulani jina nimesahau.

    ReplyDelete
  4. I_G_P na Ra-i-si wanajitahidi lakini wanaofanyakazi nao ndio balaa.
    Kwa makusudi kuna viongozi hawataki kuwajibika wanataka kuwahaibia mawazo na uzalendo wa hawa wakuu wetu.

    ReplyDelete
  5. kwa kweli mkuu tunashukuru kwa angalizo lako la kigamboni,sie kibada siku hizi hatulali,utasikia leo wamevamia kichangani,kesho uvumba,kesho kutwa shangwe etc yaani shagala bagala utadhani kigamboni hakuna polisi,na jeshi ili kwa kipande cha kigamboni wao ndo wanaosaidiana na majambazi!na sijuhi system hazioni!yaanu tunaishi kama hakuna serikali!!

    ReplyDelete
  6. kwakweli suala la usalama maeneo husika linahatarisha maisha yetu, mie naishi kibada, maisha yetu muda wote yapo hatarini, uvamizi unafanyika hata mapema mida ya kuanzia saa 12.30, watu wanakuja wanavunja nyumba zetu,wanaingia kama makwao, watu hawa wana silaha za moto, cha kushangaza polisi wanawafahamu vizuri wahusika wote wa matukio hayo. Mie ningeomba kama ikiwezekana kwakuwa kigamboni kuna kambi ya jeshi,basi jeshi liingie mtaani!

    Kifupi maisha yetu yapo hatarini sana, hatulali kama wenzetu kwa amani. Tunaomba suala hili lishughulikiwe kwa haraka. Kituo cha Polisi kigamboni kipo kama jengo tu hatujui ni lini kituo kitaanza kufanya kazi.

    ReplyDelete
  7. Mdau Mbegu nashukuru sana kwa mchango wako. Ni kweli hali ya uhalifu imeongezeka sana kwenye maeneo yaliyotajwa.
    Kwa taarifa yako kuna ujenzi wa vituo vya Polisi katika kata za Mjimwema na Kibada. Vituo hivi bado kukamilika kwani vinajengwa kwa nguvu za wananchi. Kama mdau unaombwa kuchangia juhudi hizi na kuhamasisha wengine kufanya hivyo.
    Sasa hivi niko katika ziara ya kutembelea kata. Nimekuwa nikiongoza na MaOCD tukihamasisha suala la ulinzi shirikishi. Ninaomba uwahamasishe wadau wengine katika mtaa wako washiriki katika zoezi hili.
    Dr Ndugulile-Mbunge Kigamboni

    ReplyDelete
  8. Mh.Mbunge suala la ziara za kutembelea kata na hari tete ya kibada vinawiana nini!!watu wanauawa na majmbazi kila kukicha wengine wanajeruiwa kwa kukatwa mapanga jitihada gani umefanya!!

    Sidhani kama waweza sema una taharifa na hari ya kibada!watu wanauawa na majambazi kwa kupigwa risasi,na wengine wanajeruhiwa,wanaumizwa vibaya wanaachiwa majeraha ya maisha unasema kituo hakijaisha,unataka kituo kuisha mpaka kiwekewe malumalu!! ilhari mahitaji yote ya msingi ya binadamu yapo!ikiwapo vyoo,pamoja milango,sero ya kike na kiume? n.k,sasa leo twasema bado havijakamilika wapiga kula wako wanauawa,wanajeruhiwa,wewe ukiwa kama muwakilishi wa wapigakula wasema watembelea kata!!?? hukuiwa kama mbunge watakiwa kuguswa na hari kama hii!!!!

    ReplyDelete
  9. ni kweli kituo kinajengwa pale jirani na zahanati ya kibada. tatizo jinine litakalojitokeza, baada ya ujenzi kukamilika hao polisi wataweza vipi kufika maeneo ya block 14,15 na sehemu zingine wakati barabara hazichongwa?? nathani mbunge afuatilie kwa wahusika ili barabara zitengenezwa kurahisisha miumbombinu, la sivyo tutakuwa na polisi wasioweza kufika maeneo ya watu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...