Baba wa Taifa (katikati) akiwa pamoja na waandishi wa habari wa zamani Marehemu Kanyama Chiume (kushoto) na Marehemu Robert Makange(kulia) katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam mwaka 1985 siku chache kabla ya Baba wa Taifa kustaafu Urais.
Mzee Kanyama Chiume alipata kuandikia magazeti ya Serikali ya "Nationalist" (ambalo baadaye likawa "Daily News/Sunday News") pamoja na magazeti ya Chama ya "Uhuru na Mzalendo" kuanzia miaka ya 1960 hadi ya 1980. Vile vile alikuwa columnist katika magazeti mbali mbali kama vile "Mfanyakazi", "Radi" na "Rai/Dimba" katika miaka ya 80 hadi 90. Kabla ya hapo alipigania Uhuru wa Malawi na kupata kushikilia nafasi mbali mbali za uongozi nchini humo, kama vile kuwa Waziri wa kwanza wa Elimu na Waziri wa kwanza wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo. Vile vile, alikuwa Msuluhishi wa kwanza wa mgogoro wa kisiasa huko Zanzibar kati ya ASP na ZNP chini ya usimamizi wa PAFMECA. Alikuwa muumini wa falsafa ya "Pan-Africanism" na mtunzi wa vitabu mbali mbali na mwanaharakati wa demokrasia nchini Malawi dhidi ya utawala wa kidikteta wa Rais wa Maisha wa wakati huo, Kamuzu Banda.
Mzee Robert Makange alipata kuwa mwandishi na mhariri wa gazeti la "Mwafrika" kati ya mwaka 1957 hadi 1961, gazeti ambalo lilifanya kazi kubwa ya kueneza siasa ya TANU ya kudai Uhuru. Mwaka 1958, Marehemu Mzee Makange pamoja na mmiliki mwenzake, Kheri Rashidi Baghelleh, walifungwa miezi 6 na Serikali ya mkoloni kwa tuhuma za uchochezi. Maandiko ambayo yaliwapeleka jela ni haya hapa:
"Sisi wote tunajua kuwa Mwingereza yupo hapa kwetu kwa sababu ya kutunyonya damu na kujipatia manufaa yake mwenyewe, na wala asitudanganye kwamba yupo hapa kwakuwa anatuonea huruma na kutaka kutufundisha ustaarabu au kuleta maendeleo ya nchi. Maneno haya ni kigeugeu cha kutaka kutufunika macho; na kwa kadri atakavyozidi kuwa hapa ndivyo madini na fedha zitakavyo zidi kutolewa katika nchi hii kupelekwa kwao, ambako bila ya sisi hawawezi kuishi sawasawa.“
(Mwafrika [weekly edition], No. 19, June 1st 1958, p. 5)
Mzee Makange alikuwa pia ni mtunzi wa vitabu mbali mbali kupitia kampuni ya uandishi na uchapaji ya Pan-African Publishing Company aliyoiongoza kwa miaka mingi pamoja na rafiki yake wa karibu, Mzee Kanyama Chiume.
I see Mwinyi in the background
ReplyDeleteHeshima
ReplyDeleteW Chiume
Mzee Makange pia ametuachia legacy ya "kuku makange", recipe ambayo ilianzia kwenye baa yake iliyoitwa Tropicana pale mtaa wa Nkrumah miaka ya 80s. Hizi kuku makange za siku hizi wala hazishindi ile origino yenyewe iliyokuwapo Tropicana Bar.
ReplyDelete