Picha ya pamoja baada ya Mwenyekiti  wa Taasisi ya WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kumaliza mazungumzo na ujumbe kutoka Marekani  pamoja na ungozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii
 Mama Salma Kikwete akiongea na wageni baada ya kumaliza mazungumzo.
 Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (kulia) akiagana na  Mjumbe kutoka Marekani wa Taasisi ya E G Health (kushoto) Reza Bundy baada ya kumaliza mazumgumzo na Mwenyekiti  wa Taasisi ya WAMA Mama Salma Kikwete, (pichani hayupo) Mazungumzo hayo pia yamewahusisha wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Blandina Nyoni hayupo pichani.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya WAMA Zakhia Mehgji (kulia) akibadilishana mawazo katika ofisi za WAMA jijini Dar es Salaam na wajumbe  wa taasisi ya E G Health kutoka Marekani (kushoto)ni Director, Global Programs healthymogination Joneen Uzzeli na (aliesimama katikati) ni Co- Director of African First Ladies Fellowship Program  Cora Neumann, wakati ujumbe huo ulipokwenda kumtembelea Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani ) na kuzungumzia jinsi ya kusaidia kuwaletea vifaa tiba kwaajili ya kusaidia kupunza vifo ya wakinamama na watoto wachanga nchini . 
Katibu wa Taasisi ya WAMA Daudi Nasibu (aliesimama) akitoa taarifa kwa wageni  pamoja na uongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii katika Ofisi za WAMA walipokutana na Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mama Salma Kikwete kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu kusaidia kuleta vifaa tiba kwaajili ya jitihada  za kupunguza vifo vya wakinamama na watoto wachanga nchini, Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...