Wafanyakazi wakimalizia kubandika bonge la tangazo katika jengo la Rupia kwenye mzunguko wa Msimbazi jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Wapita njia wamesikika wakihoji nini faida ya kuwa na matangazo ya aina hii yanayotumia pesa nyingi badala ya kutafuta mbadala wa tatizo bnadala ya kuendelea kunadi tatizo kwa pesa hiyo hiyo inayotupwa hapo...Bila shaka wahusika watatupa jibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. ANKO NAKUBALIANA NA HAO WAPITA NJIA KBS TENA SERIKALI IWAJIBIKE SN HUWEZI UINGIA DRS LA 3 KM HUJUI KUSOMA YANI UANZA 1 KISHA 2 HUJUI KUSOMA HADITHI KM WALIVOSEMA AFU UNAENDA LA 3 KUFANYA NINI?????? AU NDO BORA LIENDE?????

    ReplyDelete
  2. kama takwimu zinaukweli kwanini wasiweke wazi? hoja ya kutumia pesa kwa tangazo halihusiani moja kwa moja na ubora wa elimu inayotolewa,,hivyo basi pesa sio nyezo kuu ya kutatua hili tatizo bali ni uwajibikaji wa walio kwenye sekta zao..kuanzia wakuu wa wilaya,maafisa elimu ,wakaguzi wa taaluma, walimu ,wazazi na wanafunzi!! acheni kupinga kila kitu kwa kutizama upande mmoja wa shilingi!!

    ReplyDelete
  3. Unapotaka mabadiliko usiangalie gharama, hapo alieweka bango kwa gharama ambayo umesema kubwa lengo lake lilikuwa kuonyesha hali halisi ya elimu yetu hapa nchini kiasi kwamba mwanafunzi anafika darasa la tatu lakini yale aliyoyapitia darasa la pili hayawezi. Kwa maana nyingine kazi yake ni kuanzisha mjadala ili wale ambao wanajukumu la kutekeleza wajipange ili kuangalia namna ya kuondoa tatizo. Bango limewekwa kutokana na tafiti nyingi zimefanywa na kukabidhiwa serikalini lakini hazisomwi na kufanyiwa kazi hivyo hao jamaa wameamua kuweka mambo hadharani kwa umma ili mimi, wewe, wao waweka mabango na watanzania kwa ujumla tuchukue hatua.

    ReplyDelete
  4. serikali yenyewe inajitangazia ujinga?

    ReplyDelete
  5. With due respect naomba wahusika wazuie tangazo hili kwani halina faida yeyote kwa huyo mwanafunzi wa darasa la 3. Ni nani anaetowa pesa za kututukana badala ya kwenda moja kw moja kutatua tatizo? Namkumbuka sana Marehemu Julius asingekubali upuuzi kama huu.

    ReplyDelete
  6. Kwa wale waosha vinywa wasiojua Maana ya Tangazo hili ni kuifahamisha serikali na jamii ya umuhimu wa mtoto kujua kusoma .limetolewa na NGO ambayo inahamisha jamii namna kwa ufadhili wao wenyewe

    ReplyDelete
  7. ni moja ya njia za advocacy for policy change, kuna njia nyingi moja wapo ni hii wa billboards....njia kama hii sometimes inaraise voices/yaani kma kuanzisha mjadala nk kutakakoelekea kitu fulani kuwa changed. kuchukuliwa hatua nk

    ReplyDelete
  8. Hata anon wa kwanza hajui 'spelling' za kiswahili. "WALIVOSEMA" na "NDO BORA" ndio nini?

    ReplyDelete
  9. Serekali iwajibikaje???!!! wewe mzazi UJIULIZE mtoto wangu yuko la tatu bado hajui kusoma kulikoni??? WALIMU (SERIKALI) wanafanya kazi yao vizuri tusiwalaumu, darasa linawatoto 50 mwalimu atapata wapi muda wa ku-deal na watoto wenye akili nzito. WAZAZI WAWASAIDIE WATOTO NYUMBANI... hilo tangazo safi sana mgonjwa hatibiwi mpaka akubali ana huo ugonjwa na yuko tayari kutibiwa. Ukweli unauma kubali kwanza mtoto wako hajui kusoma halafu kaa chini sasa utafakari utamsaidia vipi MTOTO ajue kusoma.

    ReplyDelete
  10. Anko naunga mkono minong'ono hiyo sana, ila ukweli ni kwamba kuna wanafunzi wanaingia sekondari huku hawajui kusoma na kuandika na tunasikia kwenye vyombo vya habari.

    mi nadhani hawa jamaa wangeenda mbali na kupendekeza solution ya tatizo hilo kwani ujumbe wao una maswali mengi, kama watoto 7 kati ya 10 hawajui kusoma, so what?watanzania tunahitaji ujumbe huo uliokatika?

    Naomba serikali ikabiliane na changamoto hizo za kuboresha elimu kwani ni wajibu wao kufanya hivyo na si mashirika yasiyo ya kiserikali.
    badala ya serikali kufanya matumizi ya anasa mengi tuu kama safari zisizo kuwa na kichwa wala miguu, masherehe mengi ya kutumia mabilioni kuadhimisha miaka 50 ya uhuru huku fedha hizo zingetumika kuweka miundombinu sahihi kuwezesha mazinginra bora ya watoto wetu kujifunzia

    ReplyDelete
  11. Usijali: "NI HISANI KUTOKA KWA WATU WA................."

    ReplyDelete
  12. Tangazo linasaidia mimi kama raia kujua hivyo kama mzazi nianze kuchukua hatua na kufuatilia watoto. Vile vile kusaidia viongozi na wanaohusika kujua, kwani naamini wengi hawatambui hilo kwani sidhani kama Serikali inafanya tafiti kama hizo zaidi ya kulipa mishahara ya walimu. Hivyo tayari mi kwa kusoma hapa tu nimefaidika na hii taarifa, kuwa shule zetu zinazalisha vimeo na ni jambo la kushirikiana kwa pamoja. Wao kama wao washatupa taarifa

    ReplyDelete
  13. NI BORA KUTUMIA GHARAMA KUBWA KUWAELIMISHA WATANZANIA ILI WAJUE HALI HALISI YA NCHI YAO THEN ITAKUWA RAHISI KUTATUA MATATIZO YALIYOPO. MFANO WAZAZI WAKISOMA HILO BANGO WATAKUWA MAKINI KUWAFUATILIA WATOTO WAO AMBAO KILA SIKU WANAENDA SHULE KUMBE HAWAFUNDISHWI. NA HAPO WANANCHI WATAISHINIKIZA SERIKALI KUBORESHA HALI YA SHULE ZA TANZANIA ILI WANAFUNZI WAPATE ELIMU BORA KUTOKA KWA WALIMU BORA AMBAO WANAPATA MASLAHI MAZURI.

    ReplyDelete
  14. kila kitu kinaanza na ufahamu, kufahamu tatizo ni nusu ya kazi katika kutafuta ufumbuzi, hii ni hali halisi katika wilaya zote za Tanzania. utafiti huu kutokana na ripoti iliyotolewa, umepita wilaya zote Tanzania.

    ReplyDelete
  15. ujumbe murua kabisa,eti hizo pesa zingeenda kusaidia tatizo? nani kasema?aah mbona serikali haikubali km kuna tatizo hilo(wapi serikali imekiri uwepo wa tatizo hilo tajwa?)bango hili limebeba ujumbe wa kuibua mjadala juu ya ubora wa elimu yetu hasa kwa shule za serikali(km mtoto wako anasoma so called ENGLISH MEDIUM huwezi kuelewa sana tatizo hilo) wananchi na hasa wazazi ujumbe huu wa kwenye BANGO unapaswa kuwa chachu ya mjadala,tuchukue hatua kadri inavyowezekana kwa nafasi zetu pale tulipo,hivi hali hii ya elimu ikiendelea nini itakuwa urithi wa taifa la kesho?fikiria hao wanaosom katika shule duni zenye hali tajwa,mmh WANANCHI TUCHUKUE HATUA!BRAVO taasisi ya TWAWEZA mmendeleee hivyo hivyo!

    ReplyDelete
  16. Tusiweke Siasa mbele jamani...mi nafikiri jamaa wangetangaza suluhisho la tatizo wangekuwa kweli wameisaidia jamii na serikali kwa ujumla...lakini hili tangazo bado halijalenga ktk kuisadia jamii juu ya tatizo husika,Je ni watanzania wangapi watakaopita eneo hilo na kujua kuchambua dhima ya hilo tangazo?Ushauri wa bure kwa NGO's mi nafikiri ni wakati muafaka kuisaidia serikali yetu na sio kuikosoa kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukiikosoa na baadhi ya mambo yanakwenda poa na mengine imechemka,sasa ndio wakati wa NGO's kutekeleza dhima ya kuisaidia serikali na jamii.

    ReplyDelete
  17. Najua Michuzi hili bango limekukera kwa kuwa wewe upo kwenye kivuli cha wanaokula Neema ya nchi yetu, na hili bango kwa upande wako unaona kama linalivua nguo serikali.
    Ninaimani kila mwenye akili na mwenye kupenda maendeleo ya Taifa letu awezi kutoona umuhimu wa bango hili. ila kwa watu kama nyie mnaotaka watanzania wawe gizani ili muendelee kula mema ya Nchi kwa safari za bure zinazogaramiwa na wavuja jasho wa na masikini wa nchii hii ambao watoto wao wanakwenda shule kama sehemu ya day care badala shule kwenda shule kujifunza.
    Uwezi kufahamu umuhimu wa bango hili kwa sababu upendi kuona serikali ikivuliwa nguo

    ReplyDelete
  18. moja ya ujumbe wa hili bango ni kutufumbua macho na kutukumbusha wazazi kuwa makini na kufuatilia maendeleo ya wanetu kwa ujumla.

    ReplyDelete
  19. Wabongo tumezoea kujitetea kwa kutumia makosa ya wengine... Huu hapa mfano

    Kwani kulikua na umuhimu gani wa kulipa gharama kubwa kuweka mabango makubwa ya ankal wakati wa uchaguzi?

    Dawa ya moto ni moto....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...