Na John Kitime
Patrick anaimba wimbo ambao aliupiga kwanza akiwa na Afro70. Wimbo huu una ukweli mkubwa, unakufanya hata ufikirie kuhusu Patrick mwenyewe, kweli wema hawana maisha. Hapa Balisdya akiwa jukwaani na Shikamoo jazz. Mzee Zahoro anaonekana hapa akipiga mandolin chombo ambacho amepiga sana hasa akiwa Kiko Kids. Tunaambiwa wakati bendi zote Tabora zilianza kutumia magitaa ya umeme yeye akiwa na kiko Kids yake aliendelea kutumia Mandoline na ndio husikika katika nyimbo zake za zamani za Kiko.
Swadaktaaaaa
ReplyDeleteAhsante sana Kitime
Oh my God I had completely forgoten about Kiko Kids hahah LOL
ReplyDeleteAsante sana kaka John kwa kutukumbusha mbali. Najiona nikiwa kama miaka saba ya umri nikisikiliza hizi nyimbo na dada yangu mkubwa aliyekuwa anapenda sana kiko kids
Asnate sana John, umenikumbusha sana mjomba wangu Patrick, nyimbo alizoimba huwa zinatukumbusha sana maisha yake ya upendo, alikuwa anacheka wakati wote. RIP Patrick Balisidya
ReplyDelete