Na  US Blogger

Wadau wa globu ya jamii natumai wote wazima wa afya na munaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku.

Ninaamini wengi wenu mutakubaliana nami kwamba ushindani miongozi mwa vyama vya siasa umefikia kiwango ambacho hatujawahi kuushuhudia siku za nyuma.

Vyama vimekuwa na wapenzi wengi, wanachama wengi , mashabiki wengi na wakereketwa wengi.

Mimi ninashauri kuwepo kwa midahalo ya kisiasa miongozi mwa wanachama ama waunga mkono vyama vya siasa na midahalo hii iwe kwa ajili ya wasio wanasiasa ili tuone kama wanachama ama mashabiki kweli wana uwezo wa kutetea vyama vyao ama ushabiki wao unatokana na ushabiki pofu.

Napendekeza kuwepo kwa midahalo ndani na nje ya nchi and to get the ball rolling nje ya mipaka ya nchi walio Marekani wafungue ulingo. Midahalo iwe recorded and broadcasted ili wananchi waweze kujionea mambo yanakwendaje.

Munasemaje?

Ahsanteni.

US Blogger
Usblogger11@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. haitotusaidia

    ReplyDelete
  2. I am in. Ngoja nikasome Ilani ya chama changu kwanza

    ReplyDelete
  3. Hujasomeka mdaharo kati ya CHADEMA Vs CCM unataka iweje au wewe umeandaa nini au unafikra gani

    ReplyDelete
  4. huyu siyo mwingereza tena analeta mapepe kama kawaida. Nyie wabongo wa US mmezidi pumbaziiii

    ReplyDelete
  5. Chukua majembe mkalime, nchi haina chakula. Wachane malumbano, hakuna cha mdahalo hapa ili mje kuwamwagia watu tindikali.

    ReplyDelete
  6. HIO NDIO DUNIA ILIVYO HIVI SASA MIMI NAISHI MAJUU KWENYE KITOVU CHA DEMOKRASIA, RAIA WANAPEWA NAFASI KUBWA KUCHANGIA MAWAZO , HASA VIJANA WA VYAMA MBALIMBALI KUANZA KUJIANDAA KISIASA SIO KUVAMIA TU MAMBO AMBAYO YALIKIKWISHAPITWA TANGU 1960s NA VIONGOZI HATA TV WALIKUWA HAWANA . HIVI SASA DUNIA IMEBADILIKA. HAKUNA KINA NYERERE SIKU HIZI HATA HUYO GADDAFI NDIO MIFANO HIO MNAVYOIONA. MAREKANI KUNA MARAIS WEUSI NA MWANAMKE MWEUSI AMBAYE ANAISHI WHITE HOUSE,ANATEMBEA KAVAA KAPTULA NA ANAKWENDA KULA MC DONALD ANA JUMUIKA NA WATU WENGINE RAIS ANACHEZA BASKETBALL NA WATU TU TOFAUTI2, ULAYA NCHI KAMA ZA SCANDINAVIA MAWAZIRI WAKUU WANAENDA MAKAZINI NA BAISKELI NA HAOGOPEWI MTU. WE NEED A CHANGE

    ReplyDelete
  7. Vyama vya upinzani katika dunia ya tatu vyote sawa. CHADEMA haina tafauti na NTC au CUF au Eqypt Opposition. Hawana siasa bali choyo na husda!!!!

    ReplyDelete
  8. USELESS.

    ANZISHA BLOG YAKO HALAFU WEKA MALUMBANO HAYO.

    Kama siyo Nenda Mwananchi au Mwanahalisi.

    SABABU:
    Kila mtu atakuwa anatetea updande wake na hakua atakayekubali moja kwa moja kuwa upande wake unakasoro.

    ReplyDelete
  9. kwanini midahalo ifanyike nje ya nchi? Nchi ngapi duniani wanaofanya midahalo yao ndani ya Tanzania?

    ReplyDelete
  10. BIG UP usblogger.HII KITU NI MUHIMU SANA KWA ANAYEONA MBALI( kuleeeeeeeeeee).HACHANA NA HAO WANAO BWABWAJA BWABWAJA WANAJUA WALITETEALO KWANI HAO WATAKUWA NI WATOTO AU JAMAA NA VIGOGO VYA CHAMA TAWALA.EH BWANA ANZISHA HIYO KITU MARA MOJA MWANANGU TUMECHOKA KUKAA GIZANI,NANJAA,KWENYE NCHI YENYE UTAJIRI KM HII NDANI NA NJE YA ARDHI(madini ya tele ya aina mbalimbali,gas.petroli,uranium,tanzanite, etc.,juu inarutba ya kutosha na bado tuna njaa ajabu!!.MIAKA 50 SASA BADO TUKO GIZANI.

    ReplyDelete
  11. wengi wetu tuta furahi kuona Live Mjadala kati ya kiongozi wa CCM- Kikwete na Kiongozi wa CHADEMA Slaa.. kweye T.V, RADIO na INTERNET...!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...