Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete akipewa maelezo na Mtendaji Mkuu wa Shamba la kisasa la mpunga la Kilombero Plantation LTD Bwana Carter Coleman namna wanavyohifadhi mpunga kwa kutumia mifuko maalum ya plastic yenye uwezo wa kuhifadhi mpunga tani 105 kwa mwaka mzima bila kuharibika kwenye jana huko Mngeta, Wilaya ya Kilombero katika mkoa wa Morogoro
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akipewa maelezo na Mtendaji Mkuu wa Shamba la kisasa la mpunga linalomilikiwa na Kampuni ya Kilombero Plantation LTD Bwana Carter Coleman namna mitambo ya umwagiliaji aina ya pivot inavyoweza kumwagilia shamba na kuweka mbolea jana huko Mngeta, Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete akipewa maelezo na Meneja wa shamba Bwana Graham Anderson namna ya umwagiliaji maji aina ya 'pivot' unavyoongeza ufanisi na tija kwenye kilimo cha mpunga kwenye shamba la Kampuni ya Kilombero Plantation LTD jana huko Mngeta, Wilaya ya Kilombero katika mkoa wa Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ushauri kwa serikali ni kuwa wanaowekeza kwenye mashamba makubwa kama hayo washirikishwe katika kuendeleza na kutengeneza barabara zetu, kama huyo mwekezaji wa Kilombero basi awe mshikiri mkuu katika kunyanyua viwango vya barabara za Kilombero na maendeleo kwa ujumla...tumechoka na zawadi za vitabu bila madarasa na barabara..

    ReplyDelete
  2. Halafu kilimo cha chakula kama hiki kianze kuliwa kwanza na soko la ndani, sio hao wanauza mchele wote nje halafu sisi tunaagiza mchele wa Thailand.. maana ndio akili zetu. Mwaka mmoja tuu mvua isiponyesha tunakuwa na njaa!!

    ReplyDelete
  3. Nakuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba mchele unaotoka KPL unauzwa Tandika kama kawaida. Na, katika soko la duniamchele wa Tanzania ni gharama sana ikilinganishwa na mchele unaotoka nchi za Asia, kwa hiyo mchele wa Tanznania hauna soko sana kwa sababu ya bei yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...