Gazeti la Mwananchi, matoleo ya jana, Jumatano, Oktoba 12 na leo, Alhamisi,
Oktoba 13, 2011, limeandika habari zilizodai kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alitoa msamaha wa kupunguza adhabu ya kifo iliyowakabili askari polisi wa zamani waliopatikana na hatia ya kumpiga risasi na kumwua kwa makusudi aliyepata kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe Juni 30, 1996.
Gazeti hili limedai kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete alitoa msamaha huo kwa
kupunguza adhabu ya kifo iliyokuwa inawakabili makonstebo wapelelezi Mataba Matiku na Juma Muswa na kuibadilisha kuwa kifungo cha miaka miwili.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa Mheshimiwa Rais Kikwete hajawahi na hajapata kuhusika hata kidogo kutoa msamaha wa kirais kwa kupunguza adhabu ya wauaji hao wa Luteni Jenerali Kombe tokea kuingia madarakani.
Masuala yote yanayohusu polisi hao waliohukumiwa kifo kwa mauaji ya Luteni Jenerali Kombe yalifanyiwa maamuzi kabla ya Rais Kikwete kuingia madarakani Desemba 21, 2005.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
13 Oktoba, 2011
Embu malizieni habari, hivi wamepunuziwa adhabu na nani na wapo wapi? kuna some issues Tanzania wanazifanya kwa kutojali, wako wengi Arusha waliua sasa tuko nao mitaani ila wananchi wanataka kuwalipiza kisasi. Mbona kesi ya mwanamuzi babuseya ndo afadhali kuliko ya mauaji? Sorry ila i belive that if people meet with them probability for them to live is 50% so ithink prison is more comfortable and safe place for them to live.
ReplyDelete