wafanya biashara wadogo(machinga) wakifanya biashara karibu kabisa na mitambo ya kusambaza umeme Ubungo

Ripota wa Globu ya Jamii aliekuwa katika maeneo ya Ubungo Jijini Dar,amejionea hali isiyo ya usalama katika maeneo hayo ambapo wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga wamekuwa wakifanya biashara katika mazingira hatarishi sana hasa ukizingatia kuwa eneo hilo limezungukwa na mitambo ya kuzalisha na kusambaza umeme jambo ambalo ni hatari sana kwa maisha ya wafanya biashara hao,lakini pia waendao kwa miguu na wanunuzi.

 Hatari hiyo inatokana na ukweli kwamba watu huwa wengi jioni katika eneo hilo jambo linaweza kusababisha maafa makubwa sana iwapo janga la moto litatokea katika eneo hilo.

Daima kinga ni bora kuliko tiba hivyo ni ombi letu kwa serikali kuliangalia jambo hili kwa upana zaidi ikiwa ni pamoja na kupitia alama za kiusalama ili kuepusha janga lolote kutokea katika eneo hilo badala ya kusubiri janga kutokea ndipo ikumbukwe kuunda tume ya kuchunguza wakati tayari maisha ya watu wasio na hatia yatakuwa yamepotea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Mheshimiwa Michuzi, serikali inasubili kwanza maafa yatokee ili yaundiwe tume ya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tatizo

    ReplyDelete
  2. hapo kwa Mnyika, ukiwatoa tu ataanza kelele not knowing kwamba kukaa chini ya hizo nyaya za high voltage kunasababisha kansa.

    ReplyDelete
  3. Mukiwaambia hiyo mionzi inaharibu 'Ofisi' (mfumo wa uzazi) hao watakimbia wenyewe.

    Stori za kansa haziivi kwa Wabongo.

    ReplyDelete
  4. Tunashukuru kwa kuendelea kuliona hili.Mimi naishi Finland,japo pia nimetembelea Uganda,kenya ,Spain,Russia,Norway na Marekani tena miji mikubwa ya nchi hizo.
    Knachonistikitisha ni kuona mitambo ya kusambaza umeme mji mzima inaendelea kuboreshwa na kurundikwa katikati ya mji Ubungo.Unajuwa watu wasioipenda nchi yetu wakiamua kuitumia kama siraha-HATA IKURU KIVUKONI ITARIPUKA KWA SABABU YA MITAMBO HIYO,MAANA HAPO KUNA MITUNGI YA GESI MIKUBWA NA BOMBA PANDE ZOTE MBILI.
    Hakuna anyeonyesha kujari,angalau basi waihamishie Chalinze,Tegeta,au Mbezi.wanatoa maeneo makubwa kwa wawekezaji tena kwa fedha nyingi ila wanasahu usalama.WHEN SAFETY IS SUBJECTED TO MONEY,THE NATION IS DYING.

    ReplyDelete
  5. michuzi tatizo sio serikali tatizo ni hali ya siasa nchini mwetu hao watu ukiwaondoa hapo kwa nguvu kunawatu wanaojua kuchana na kurepu kwa faida ya vyama vyao watakuja juu na kuanza kusema serikali inawanyanyasa waache kwanza ili litakapo tokea tena ni hao hao wanaotafuta umaarufu ndio wakwanza kuchonga tena jamani hii siasa imefikia sehem sasa kwa mtu mwenye akili na mtazamo hawazi kumsikiliza hata mwanasiasa mmoja kwani wote waoongo tu wanataka kuungwa mkono kwa maslahi yao binafsi mungu aibariki sana nchi hiyo

    ReplyDelete
  6. Tena hawa wanaoonekana pichani ni wachache sana. Hebu pita hapo usiku kati ya saa 1 na 4 ujionee jinsi watu walivyosongamana hadi watembea kwa miguu wanalazimika kupita barabarani.Hapa hakuna cha Mnyika wala nini. Hawa wanapaswa kuondolewa. Tusilete siasa kwenye usalama wa watu.

    ReplyDelete
  7. Umeme wenyewe hamna,wasi wasi wenu ni nini?

    ReplyDelete
  8. wewe finland ndio kukaa ulaya sana au? unaweka ma rrrr bila mpango huwa mnaboa sana, ikuru-ikulu, siraha-silaha, itaripuka-italipuka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...