Uongozi wa ASET kupitia Bendi yake ya AFRICAN STARS “Twanga Pepeta” inatarajia kufanya Tamasha kubwa litakaloitwa “Twanga Festival” au Tamasha la Twanga.

Tamasha la Twanga litahusisha kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara na uzinduzi wa albamu ya 11 ya Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta”.

Tamasha linataraji kufanyika siku ya Jumapili tarehe 06-11-2011 katika viwanja vya Leaders Club vilivyopo Kinondoni.

Shamrashamra ya Tamasha zitaanza kwa mashindano maalum ya mchezo wa soka kwa kushirikisha timu 12 za maveterani. Mashindano hayo yatajulikana kwa jina la “VETERAN ASET FOOTBALL TOURNAMENT” na timu zitakazoshiriki ni pamoja na wenyeji wa mashindano Twanga Pepeta FC, Brake Point FC, Mango Garden FC, Singasinga FC, Namanga FC, Kigamboni FC na Ukonga FC, nyingine ni Mango Taxi Drivers FC, Mpilipili FC, BM FC. Leaders FC na Daladala camp FC.

Mashindano yatakuwa yakichezewa katika Viwanja vya Leaders Club na yanategemea kuanza siku ya jumamosi ya tarehe 15-10-2011 na kumalizika siku ya  ya Tamasha tarehe 06-11-2011.

Nyimbo zitazokuwa kwenye albamu hiyo ni sita ambazo ni  “Mapenzi Hayana Kiapo” uliotungwa na Saleh Kupaza, “Mtoto wa Mwisho” uliotungwa na Ramadhani Athumani au Dogo Rama, “Penzi la Shemeji” uliotungwa na Mwinjuma Muumini, “umenivika Umasikini” uliotungwa na Luizer Mbutu, “Dunia Daraja” na nyimbo “Kauli” iliyotungwa na Rogart Hegga.

Kabla ya uzinduzi kutakuwa na “Red Carpet Listening Party” maalum kwa ajili ya wadau mbalimbali kama Waandishi wa Habari, wamiliki wa Stesheni mbalimbali za Radio na TV, wanamichezo mbalimbali, wanasiasa, wacheza filamu, wabunge na Mameya wa manispaa zote tatu za Jiji la Dar es salaam, Mashirika ya Hifadhi ya Jamii kama NSSF,PPF, Benki mbalimbali kama NBC, Akiba Commercial na Benki ya wanawake. Wizara ya Kazi na Ajira, wizara ya utamaduni na michezo, Wizara ya wanawake na watoto, Wizara ya Viwanda na Biashara, Makampuni ya simu VODAACOM, AIRTEL, TIGO, ZANTEL,SASATEL,TTCL, COSOTA, BASATA, Makampuni mbalimbali kama TBL, SBL, T.C.C, TDL NA ngos  kualikwa kwa pamoja kwa ajili ya kuzisikiliza nyimbo mpya zote sita na baadhi ya nyimbo zilizopita ambazo zilibeba majina ya albamu. Nyimbo hizo ni
01.              Kisa cha Mpemba.
02.              Mtu Pesa.
03.              Safari 2005.
04.              Mwana Dar es salaam.

Albamu 10 zilizopita za Twanga Pepeta ni Kisa cha Mpemba iliyozinduliwa mwaka 1999, Jirani ilizinduliwa mwaka 2000, Fainali Uzeeni ilizinduliwa mwaka 2001, Chuki Binafsi ilizinduliwa mwaka 2002, Ukubwa jiwe ilizinduliwa mnamo mwaka 2003, 2004 ikazinduliwa Mtu Pesa, 2005 ilizinduliwa Safari 2005, Password ilizinduliwa 2006, 2008 ilizinduliwa Mtaa wa kwanza na Mwaka 2010 ilizinduliwa Mwana Dar es salaam.

Maandalizi kwa ajili ya Tamasha yanaendelea vizuri na Bendi itaingia Kambini itakayotafutwa hapo baadae. Tamasha linataraji kupambwa na wasanii wa fani mbalimbali kama Taarabu, Muziki wa Dansi na Muziki wa kizazi kipya.
  
ASHA BARAKA
MKURUGENZI ASET.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. IMEKAA VIZURI HIYO, HONGERENI TWANGA KWA KAZI ZENU NZURI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...