Wazazi wakionekana kufurahi na watoto wao katika mkusanyiko huo uliokutanisha Familia za Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kucheza pamoja, kula pamoja, kunywa pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.
Mgeni rasmi Mkuu wa Itifaki Balozi A. Itatiro akizungumza machache wakati wa UN Family Day na kusema kwamba siku hiyo haikuwa ya kusoma risala bali ni siku ya kufurahi pamoja....Happy Birthday UN..!!!
Ilifika zamu ya Wakubwa kupimana nguvu katika mchezo wa kuvuta kamba baina ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Pichani juu ni mmoja wa wachezaji nyota wa wizara hiyo, Shaaban Kessy Mtambo, akihamasisha wenzie katika mchezo wa kuvuta kamba.
Kapteni wa timu ya Mpira wa Miguu ya Umoja wa Mataifa akipokea kikombe cha ushindi wakati wa mchezo wa kuvuta kamba kwa niaba ya wafanyakazi wenzake kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa Itifika Balozi A. Itatiro. Chini UN Oyeee....
Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika picha ya pamoja na kikombe chao.
Ni wakati wa kucheza Kwaito.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...