Wana jumuiya ya Watanzania wa New York City wakiwa kwene hafla  ya kumuaga mwana jumuiya mwenzao Bi Mosi (mbele kati). Nyuma ni Ustazi wetu hapa New York bwana Mafta, na dada zetu Adela na Asya mwilima. Pia kiongozi wa jumuiya  bwana Shaban Mseba (mbele kulia) na mai hazbendi wa Bi Mosi mwenye kofia shoto
 Bi Mosi na wadau wa New York
BI MOSI katikati akiwa na mumewe waliandaliwa hafla  hiyo na wana jumuiya  wa New York City kama ishara ya upendo juu yake kutokana na jinsi alivyoishi nao na kushirikiana nao kwa kila jambo akiwa hapa. Hafla  hiyo ilihudhuliwa pia na viongozi wa jumuiya ya watanzania waishio New York City na vitongoji vyake. Kwa upande wa ubalozi uliwakilishwa na mama Rose Mkapa..Bi Mosi anarudi Nyumbani Tanzania na moja kwa moja baada ya kuishi New york kwa miaka isiyopungua 25. Na akiwa Tanzania ataelekea kwenda kuisha katika kitongoji cha Vikokotoni huko Zanzibar. Hakika  wanajumuiya watamkosa sana mama huyu kwani alikuwa ni mpikaji  mzuri sana wa vitumbua na maanjumanti mengine pale unapotoa order. Na yeye akiwa na muda wakufanya hivyo baada ya kazi zake za kila siku.  Wanajumuiya  wanamtakia safari njema na afya njema uko endako. 
Picha na wadau Sophia na Ny Ebra wa New York City.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...