Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Stellah Kiwango akitoa mada kuhusu Uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi tofauti ya watu katika Mkutano wa siku moja ulioshirikisha wafanyakazi wa idara mbalimbali za Kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Stellah Kiwango (kushoto) akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wenzake ikiwa ni sehemu ya utambulisho wakati wa Mkutano wa siku moja wa Uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi mbalimbali ya watu uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa masuala ya uongozi ambao pia ni wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimisha mkutano wao wa siku moja uliofanyika jijni Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom kutoka Idara mbalimbali wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa katika mkutano wa uongozi na nama ya kufanya kazi na makundi mbalimbali ya watu uliofanyika jana jijini dar es salaam.
Mmoja wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Bw. Charles Erasto akiuliza swali juu ya mada zilizojadiliwa katika mkutano ulioshirikisha wafanyakazi wa idara mbalimbali za Kampuni hiyo wa uongozi na namna ya kufanya kazi na makundi tofauti ya watu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hii ni taarifa nzuri. Nashughulikia sana hiyo mada huku Marekani kwa mihadhara na warsha, na Tanzania pia nimeshafanya warsha kadhaa. Dunia ya utandawazi wa leo inahitaji sana umakini katika masuala hayo. Niko tayari kuwasiliana na wadau wengine ili kubadilishana uzoefu na mawazo.

    ReplyDelete
  2. Kaka Chale....!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...