Mtoto Zahra Omar Awesu (Miezi 6) anayeugua Ugonjwa wa Moyo ambaye pia ni miongoni mwa watoto wanaotarajiwa kwenda Nchini India kwa matibabu (Picha na Hamad Hija-Maelezo Zanzibar)

Na Fatma Mzee-Maelezo Zanzibar

Wagonjwa wa Moyo 611 kati ya 1000 wanatarajiwa kuondoka Zanzibar kwenda nchini India kufanyiwa matibabu ambapo kati ya wagonjwa hao wengi wao ni watoto wenye umri chini ya miaka kumi na mbili.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Omar Abdalla Ali wakati alipokuwa akimkaribisha Hoyce Temu ambae aliwahi kuwa Mrembo wa Tanzani mwaka 1999 kwa lengo la kuwaona wagonjwa hao ili aweze kuwashawishi watu wenye uwezo kusaidia matibabu ya wagonjwa hao.

Katibu huyo alisema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walifanikiwa kuwapeleka wagonjwa 662 nchini Izraeli na wagonjwa 125 kupelekwa India kwa matibabu ya Ugonjwa wa Moyo katika miaka iliyopita.

Aidha aliwataka wadau mbalimbali wenye uwezo kuzidi kulitilia mkazo suala la kuchangi matibabu kwa watu wenye mahitaji ili kuisaidia Serikali katika kukabiliana na matatizo ya kiafya kwa wananchi wake.

Kwa upande wake Mrembo huyo wa Tanzania Hoyce Temu aliwaahidi wazazi wa watoto wenye matatizo ya moyo kuwa atatumia nguvu zake zote kwenda kuwashawishi watu wenye uwezo ili kuhakikisha wanachangia huduma za matibabu kwa wagonjwa hao.

Aidha Hoyce Temu alisema kuwa atarudi Zanzibar baada ya Wiki Moja ili kuleta mchango wowote atakaofanikiwa kuukusanya kutoka kwa wadau mbalimbali ili uweze kusaidia katika Safari ya hiyo ya India.

Amesema atakapo rudi Zanzibar ataanza na safari ya watoto sita ambao watakuwa na hali mbaya zaidi huku wengine wakisubiri kupatikana msaada ili nao wapelekwe huko India.

Aidha Mrembo huyo aliaahidi pia kushirikiana na Madaktari wa Mmanazi Mmoja na wazazi hao ili kuhakikisha tatizo hilo linaweza kupunguwa kwa kiasi kikubwa.
Amewataka Wazanzibari wenye uwezo kulichukulia umuhimu suala hilo ili kuweza kusaidia wanyonge na watu watu wasikuwa na uwezo wa kuwapeleka watoto wao matibabuni.

Nao baadhi ya wazazi wa watoto hao walimshukuru Hoyce Temu kwa ahadi zake na kuwaomba watu wenye uwezo hasa kwa kwa upande wa Zanzibar kusaidia watoto hao kwa hali na mali kwani fungu lao kubwa litabaki kuwa kwa Mungu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ni jambo zuri lakini binafsi sijafurahia hiyo picha inamuonyesha mtoto mdogo sana lakini amepakwa wanja hujamtendea haki mtoto au niko wrong mnaonaje wenzangu....

    ReplyDelete
  2. Kupakwa wanja kwa mtoto mchanga ni utamaduni wetu hauna uhusiano wo wote na ugonjwa alio nao.

    ReplyDelete
  3. mimi nimefurahi sana kusikia hiyo safari ya wagonjwa,lakini nauliza hivi wagonjwa 1000 kuwasafirisha na kuwaleta madaktari mabingwa hapo nyumbani kipi rahisi?hata mabingwa hao wakiwa 20 na vifaa vyao bado rahisi sana kuliko kuwasafirisha india na wakisha fanyiwa dawa hapo nyumbani familiya zao zipo kapo karibu nao kwa uangali,zi zaidi,samahani kama mawazo yangu yatakuwa wrong na yawengine niya ni kutibiwa wagonjwa wetu,mungu awapeleke salama na matibabu yawe mazuri amin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...