NA SALAMA NJANI NA JUMA MMANGA -BEIJING CHINA
Zanzibar imetajwa kuwa ni nchi moja wapo yenye mashirikiano mazuri na China kimaendeleo hasa katika nyanja ya sayansi na teknologia kwa vyombo vya habari vya radio na televisheni .
Zanzibar imetajwa kuwa ni nchi moja wapo yenye mashirikiano mazuri na China kimaendeleo hasa katika nyanja ya sayansi na teknologia kwa vyombo vya habari vya radio na televisheni .
Akifungua Warsha ya teknolojia ya utangazaji kwa nchi zinazoendela za Afrika,Mkurugenzi mwendeshaji wa China Radio na Televisheni (CRTV) Li Jinrong leo,amesema Zanzibar imekuwa ni rafiki na mshirika wa siku nyingi ikiringanishwa na nchi nyingine za Afrika katika ukuzaji wa teknolojia ya habari ambayo ni muhimu kwa dunia ya sasa ya sayansi na teknolojia.
Amesema vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kuhakikisha vinaenda sambamba na sayansi na teknolojia kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa jamii na kuharakisha harakati za maendeleo.
Jinrong ambaye ni Mhandisi amesisitiza kuwa mashirikiano yao na nchi zinazoendelea za Afrika ni njia moja ya kubadilishana uzoefu wa matumizi yateknolojia ili kuleta uwiano wa mfumo wa Dunia wa teknolojia hasa katika vyombo vya habari.
Amesema kwa sasa China imeandaa miradi zaidi ya Elfu Moja ikilenga kutoa elimu kwa nchi za Afrika kuhusiana na sayansi na teknolojia kwa vyombo vya radio na televisheni.
aidha China imefanikiwa katika usambazaji wa mitambo ya masafa mafupi (Short Wave) na masafa ya kati (Medium Wave) pamoja na kutoa mafunzo kwa watendaji wa vyombo vya habari.
Pia China ina miradi mbali mbali ambayo inazifikia nchi mbali mbali za Afrika na duniani kote. Mhandisi Jirong amefahamisha kuwa lengo la miradi hiyo ni kubadilishana uzoefu wa kiutendaji wa kazi za kiteknolojia pamoja na kudumisha mashirikiano kati yao na nchi nyingine katika tasnia ya habari.
Warsha hiyo ya Wiki Mbili inayowashirikisha wanahabari kutoka vyombo vya habari vya Afrika ikiwemo Tanzania Bara Zanzibar,Malawi,Botswana,Congo,Ethiopia,Cambodia na China yenyewe inafanyika mjini Beijing China.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...