Mkuu wa mkoa wa Kigoma Luteni Mstaafu Issa Machibya akiwatabulisha wageni muhimu kutoka Rwanda na Burundi walipokuja kushuhudia kuanza kwa huduma za ndege ya ATC kwenye mikoa ya Kigoma na Tabora jana.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mkurugenzi Mkuu wa ATC, Paul Chizi (mwenye suti nyeupe) akikata keki kabla ya safari kuanza katika uwanja wa Kimataifa wa JK Nyerere.
 Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.
 Abiria wakipanda ndege ktk uwanja wa JK Nyerere kuelekea Kigoma.
Abiria kutoka Tabora wakishuka kwenye ndege ktk Uwanja wa Kimataifa wa Jk Nyerere jijini  Dar es Salaam jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. ATCL karibuni sana ..poleni na yaliyowasibu...msikubali tena kurudi huko mlikokuwa mmefika..lakini bila kuwa na ndege kubwa za kisasa mtachemsha tu(Long range jets).Tunahitaji mtoke nje ya nchi jamani..nasisi tutembee vifua mbele huko nje ya nchi.."The wings of Kilimanjaro"..karibuni sana sana..

    Website yenu...!!


    David V

    ReplyDelete
  2. Kaka Mithupu,

    Thanks for the pics/report. Labda kwa kusahihishana tu, hii ndege siyo mpya ( in miaka 14 hewani), imeshatumiwa/kukodishwa na makampuni mengine matano kabla ya ATCL. Vilevile siyo mpya kwa ATCL, walishaikodishwa mwaka 2008.

    Source: http://www.planespotters.net/Production_List/De-Havilland-Canada/DHC-8_Dash-8/462,5H-MWG-Air-Tanzania.php

    Kaka YeNu.

    ReplyDelete
  3. Hivi ni lini na sisi tutaweza kuwa na ndege itakayo fika mpaka nchi za ulaya na kwingine.Ndio maana nchi yetu haitambuliki kama Kenya.

    ReplyDelete
  4. Hivi kweli bongo tunacheza! Miaka 50 ya Uhuru nchi haijawahi kuingia vita amani mustarehe, hadi leo hii hatuna shirika imara la ndege???
    Halafu tunataka kuimarisha utalii, itawezekana vipi wakati hata hizo ndege(kibebeo) cha kuwaleta watalii hatuna.
    Ndege huchangia kiasi kikubwa kuitangaza nchi nk.
    Tuone Ethiopia Airline, Kenya Airways, South Africa Airways, nk.
    Tuache uhuni jamani dunia imeshatuacha mbali sana, tuamke tukimbia mchakamchaka, tuache mambo ya mzaha!

    ReplyDelete
  5. Najisikitikia mimi kama kijana wa kitanzania. Nchi yangu mpaka leo shirika la ndege la maana haina. Dunia hii ya leo??? ambapo kila watu wanajitahidi kupaa dunia nzima, sisi bado Tabora pia tunafika kwa shida. Kama ni kweli mtoto wa nyoka ni nyoka basi mimi kijana wa leo future yangu iko hatiani. Usijiulize mengi hebu tazama hizi website za majirani zetu halafu ulinganishe huduma zao na zetu(kwanza website ya Air Tanzania mpaka leo hii haifunguki AIBU KUBWA)Mwezi na nusu uliopita umeme ulikatika airport Dar abiria kutoka nchi za ulaya wakalazimika kusubiri saa nzima ya nyongeza Nairobi. Rafiki yangu aliyekuwemo kwenye safari ile nilikosa ya kumweleza kwa kweli.Aibu yote akanibebesha mimi, nami nikaikubali kwa kuwa Tanzania ndiyo kwetu. Wacha tusubiri miujiza labda kuna siku tutaamka asubuhi tushuhudie Air Tanzania ikipaa kuelekea New York,Sydney au Moscow direct kutoka Dar Es Salaam. Sijui kama kuna kiongozi yeyote aliyeko hapo Air Tanzania mwenye dreams kama hizi. Kila kitu kinaanza kwa kudream halafu munafanya kweli. Anyway pitia pitia hizi links utazame na wewe wenzetu wanavyojitahidi kwenda na wakati. Tuwashukuru Precision Airways angalau kutufuta machozi.Big up Precision Air.
    http://airtanzania.com/(Air Uvundo)
    http://www.airmalawi.com/
    http://www.kenya-airways.com/home/
    http://www.air-uganda.com/
    http://www.rwandair.com/
    http://www.flyzambezi.com/
    http://www.flyethiopian.com/

    ReplyDelete
  6. jamani dodoma na penyewe tunahitaji ndege.....hata mara moja kwa wiki

    ReplyDelete
  7. eti nini??? kadege kapya!!!! haka ni kadalili kema...??? teh teh teh...big up guys..

    ReplyDelete
  8. eti nini??? kadege kapya!!!! haka ni kadalili kema...??? teh teh teh...big up guys..

    ReplyDelete
  9. aisee ni aibu...tanzania tutabaki na siasa zetu tu..ukiwa unatoka ugaibuni ukipita uwanja wa kenya utaona Kenya airways kibao uwanjani tena kubwa balaaa.....Sasa shuka jk nyerere!haahaaaa ngja nicheke kwanza maana ni aibu tu uwanja haina ndege za nyumbani hata moja!!Sahv wamezindua boeng 787 ya plastic sisi ndo kwanza tunakodisha vibajaj tutafika kweli?mmh!!kazi ipo maana zamani Air Tanzania ilikuwa na ndege za uhakika hadi mwili wa mwalimu ulifuatwa na ndege yetu.Leo akifa mkubwa itabidi tuombe ndege maana sisi hatuna.


    David Muni-Mansita

    ReplyDelete
  10. hiyo ndege si mpya bana..
    Waache mambo hizo.. Tatizo tunaongea sana kuliko vitendo hiyo ndege kuruka jana tu, viongozi wa Serikali wanaanza kuidoea kupanda bure.
    Ndege iliyopata ajali mwanza wameshindwa kuitengeneza kununua mpya wataweza?

    ReplyDelete
  11. Hakuna cha kusherehekea hapo!! Ni aibu tupu taifa zima limeshindwa kuwa na shirika la kuaminika na kumiliki ndege ya kikweli! Kwa wadau wa mambo ya usafiri wa anga, hiyo ni sawa na kulinganisha kuwa na ki Bajaj kilichotumika wakati wenzako wana ma Scania mapya kibao!! Inaumiza roho Watanzania tunavyozinguliwa na Watanzania wenzao!

    ReplyDelete
  12. Very Good News.HONGERA ATCL. BUT.....
    1.no credits for anybody even the government because they will not pay.

    2.strict administration

    3.very strong finance control daytoday.

    4.reasonable tariffs.

    5.Stick to schedules.

    6.Staff must be polite very polite.

    7.No more free flyers on ATCL.

    Welcome back to our skies.

    ReplyDelete
  13. nakumbuka miaka ya 90 kulikuwa na ndege moja ya tanzania ukipita juu lazima uijuwe kama hiyo ni air tanzania maana ilikuwa na mlio wake utasema gari lililopasuka exsosi hahahaha

    ReplyDelete
  14. Subirini muibe rasilmali za Zanzibar ndio mtanunua ndege mpya. Hasidi siku zote habariki. Tanganyika toka kwa muasisi wake Nyerere haikuwa na haja ya kushughulikia maendeleo ya nchi yake badala yake wameendeleza uhasidi kuhakikisha Zanzibar haiendelei tu. Ok sisi tuko nyuma lakini na nyie hamna mnapofika.

    ReplyDelete
  15. Hwa bwana ni wabababhishaji sana: Tunawadaia nauli za watoto wetu toka Mwanza toka mwaka jana waliposhindwa kuruka toka Mwanza, sasa wanamaliza pesa kwa kukata keki! Zaidi wanazo Ndege Mbili wafanyakazi zaidi ya 3500 wapi na wapi.

    ReplyDelete
  16. hawa jamaa wana utani website gani inabidi ulogin na hamna sehemu ya kujiandikisha.

    http://www.airtanzania.com/src/login.php

    hamna kitu hapo ni utani tu.

    ReplyDelete
  17. Du! alhamdulilah wamefika salama

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...