Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipozi na kamati maalum ya CHADEMA ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh Freeman Mbowe pamoja na baadshi ya mawaziri leo Ikulu jijini Dar es salaam kuzungumzia mchakato wa katiba. stori kamili na mapicha kibao baadae....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Safi sana! Watanzania lazima tukubali kuwa maana ya demokrasia ni kukubali kutofautiana bila kuchukiana. Watanzania wote tuko katika jahazi moja safarini pamoja. Tutafika ikiwa sisi wote tutafanya kazi pamoja licha ya tofauti zetu za kisiasa, kikabila, kirangi na kidini. Nawapongeza viongozi wa CCM na Chadema kwa hatua hii ya mdahalo wenye nia ya kulisaidia taifa letu. Mungu ibariki Tanzania. Agustino, Njiro, Arusha.

    ReplyDelete
  2. Hii ni political asset kwa Chadema na President himself (not CCM!) na political liability kwa vyama vingine vya upinzani. I love the game of politics :)

    ReplyDelete
  3. This is a first step in the right direction. Good initiative!

    ReplyDelete
  4. Hongera sana Mh RAIS JK kwa kukubali ombi la CHADEMA Huu ndio utawala tunaotaka ktk nchi yetu tupingane kwa hoja
    Mfano huo ufuatwe hata pia na wakuu wa mikoa,RPC,mawaziri kukubali kukutana na watu wengine kwa ajli ya maslahi ya taifa letu
    Imetulia hiii nimeipenda sana

    ReplyDelete
  5. hizo kombati anapendeza mbowe, mdee, mnyika, grace na lema wengine sijui wanashonea wapi..

    ReplyDelete
  6. Rais amefanya jambo la hekima sana hii ndo tafsiri kamili ya demokrasia ya kweli! Ameonyesha ni jinsi gani amekomaa kisiasa. Siasa ni compromise sio uadui kwani wote sisi watanzania ni watu tunaoishi katika nchi moja na tunaipenda nchi yetu na tunatamani amani iendelee kuwepo na mwananchi awe na maisha nafuu angalau kupata mahitaji muhimu, Afya, Elimu bora, Chukula bora na makazi bora, mengine ni ya ziada. Kwa mtindo huu rais anatakiwa kumaliza kabisa migogoro inayoendelea Arusha kwani inakera sana inapojirudiarudi! na akiachia polisi kuendelea kutatua kwa kutumia nguvu damu zaidi itamwagika hatuombei litotee hilo ila kama akikaa kimya na asipoongea kama alivyoongea hayo yanauwezekano yakatokea. Ni jambo la kufurahisha kuona kwamba wanasiasa wanakaa meza moja na wanajadili mema ya nchi yao.
    Mungu azidi kuibariki Tanzania,

    ReplyDelete
  7. is this a brain wash or real maana siyo watu wanapiga kelele na weingine wanakamtwa na kutiwa ndani kwa kusema ukweli. Kama CCM keli wanaweza kuwa wakweli na kuto tumia njama zao na ubabe kwenye uchaguzi basi itakuwa ni hatua ya kwanza na bado nyingine kufuatia. Lakini isiwe chama kimoja tuu kinapewa chance kama hii inabidi na vingine navyo vipewe haki yao na wao wakutane na raisi kuhusu swala hilo pia

    ReplyDelete
  8. Hamna kitu hapo ni chumvi chumvi tu ka kupuliza kwa panya wakati kaing'ata kisigino.siasa ni mchezo mchafu.

    ReplyDelete
  9. Dai michuzi umetuahidi mapicha kibao baadae. Nimeisubiri hiyo baadae mpaka nimechoka. Tuna hamu kusikia yaliyojiri kwenye huo mkutano.

    ReplyDelete
  10. Tusubiri tuu hapo mkianza kuumuka kaa kitumbua mtajua...

    ReplyDelete
  11. Wewe anony wa Nov. 27, 09: 31: 00pm
    Kama una chama chako kinataka kuonana na Jk, nadhani unaweza kutuma maombi kuliko kulalamikia chooni.

    ReplyDelete
  12. Sina tatizo na timu ya Chadema, tatizo hapo ni timu ya JK, Huyo Tyson na Lukuvi bure kabisa hawawezi kumshauri kitu kizuri JK hata siku moja. Kama mnabisha subirini. Hata hivyo ni hatua nzuri ya kuanzia.

    ReplyDelete
  13. Ahsante sana...sasa ndio tutajua waliokuwa na nia mbaya na mustakabali wa nchi yetu kwa kufurahia kutokuelewana kisiasa mzizi wa fitna umekatika,,,wakae wakijua kuwa ''mwisho wa ubaya ni aibu''

    ReplyDelete
  14. Nchukua nafasi hii kumpongeza mheshimiwa Rais kwa kukutana na ujumbe wa chadema,wakati huo huo kuwakumbusha chadema kuwa JK ndio rais wetu pamoja na kuwa walitoka nje wakati mheshimiwa rais alipohutubia bunge.Hakuweka kinyongo ,hii inaonyesha ukomavu kisiasa.

    ReplyDelete
  15. HONGERA MHESHIMIWA JK, KWA HILI UNASTAHILI PONGEZI MHESHIMIWA RAIS.

    RAI YANGU NI KWAMBA, TAFADHALI SANA MHESHIKIWA RAIS, NENDA PIA ARUSHA, KAMALIZE MTAFARUKU. MIMI NASEMA UNAWEZA MHESHIMIWA, KABISAAAAA. CHUKUWA NAFASI YAKO KAMA ULIVYOFANYA LEO, WASAIDIZI WAKO HAWAWEZI, WANAKUSABABISHIA DOSARI, KUMBE SIVYO ULIVYO.

    SI ULIWASIKIA WAKIKUPANGIA KUWA PIA UUNGANISHE NA VYAMA VINGINE!!! WALITAKA PASIKALIKE WALA PASITOSHE!! NAKUSHUKURU SANA, ULILIONA HILO MAPEMA.
    NARUDIA TENA, HONGERA MHESHIMIWA.

    NAKUMBUKA ULISEMA UNATAKA KUFANYA MAMBO AMBAYO BAADAYE WATU WATAKUKUMBUKA, NADHANI DHAMIRA YAKO INAONEKANA. SASA NENDA ARUSHA. KWA NINI MR 2 AWEZE KUTULIZA WATU MBEYA!! UTASHINDWA WEWE, SIDHANI. ARUSHA KUNATAKIWA BUSARA TU KAMA HIVI ULIVYOFANYA, BASI, WALA SII NGUVU.
    NAKUOMBEA KWA MUNGU AKUZIDISHIE BUSARA, HEKIMA NA KUKUONGOZA VEMA KATIKA KUIPELEKA PEMA NCHI YETU NZURI YA TANZANIA. AMEN.

    UPO USEMI UNSEMA "HEKIMA HUVUTA WENGI". JAMBO HILI LIMEVUTA WATU WENGI SANA NAKUAMBIA. JAMBO HILI LIMEZIDI KUJENGA UMOJA WA NCHI.

    MUNGU AKUBARIKI SANA RAIS WETU NA AKUZIDISHIE UPEO ZAIDI WA BUSARA.

    ReplyDelete
  16. this is wot we koll good governance.lazima kuwepo na negotiations on kila kitu.iyikadi zipo ila zitumike kujenga nchi.suyo kila mara kuwa na fikra eti chadema au rais no mbaya.lazima kusikilizana na kukubaliana.hao wasaidizi wa rais fukuza kazi...wapotoshaji wakubwa wa habari.

    ReplyDelete
  17. Tumeshuhudia yanatimia sasa...pana tofauti kubwa sana tu kati ya Siasa za Ki Banyamulenge na Siasa safi za kistaarabu za Ki-Tanzania...tumekomaa sana ki siasa na kila tofauti inatatuliwa ktk njia ya maridhiano pande mbili kama hivi!!!.

    ReplyDelete
  18. JK ukimaliza, hapo tunataka utusainie muswaada, tuedelee na mchakato wa katiba! Hao jamaa wanajifanya 'nationalists' huku wanaitenga jamii moja kubwa hapa nchini. kwa vile huu ni mfumo wa 'one person, one vote' hawatawali nchi hii..wasikutishe!1

    ReplyDelete
  19. wewe anony wa Nov. 28 , 06:26:00 AM 2011. inaelekea huelewi kusoma na ndiyo nyinyi wapaukaji na ndiyo maana hatutafika mbali lakini sina lakusema kuhusu wewe maana haufikiri outside the box.

    ReplyDelete
  20. Mbona mibaba mitupu akina mama wako wapi?

    Mmoja, wawili ....... basi

    ReplyDelete
  21. CDM kwa pamoja wanacheka kwa furaha sana hapo, wamemuona raisi.

    ReplyDelete
  22. Upevu wa kisiasa, tunajenga nyumba moja haina haja ya kugombania fito.

    Wise Move kwa Raisi na CDM

    ReplyDelete
  23. Ndio picha inafurahisha sana kuona 1.UONGOZI WA WATU MIKONONI MWA WATU ,
    2.AMBAPO KILA KINACHO WAHUSU WATU,
    KINAJADILIWA NA WATU,
    3.KWA MANUFAA YA WATU WOTE, NA KUHESHIMU WATU KWA WATU,
    4.KWA FAIDA YA WATU, NA MWISHO WATU WANAPIGA HATUA MBELE KWA KUTHAMINIANA WATU KWA WATU...

    Hii ndio Siasa yenye TIJA na huku ndio kupevuka kisiasa!

    Hongera sana RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA WANA CHADEMA!!!.

    ReplyDelete
  24. Hii ndio aina ya siasa ambayo tunaitaka ktk JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA!

    Na sio Siasa za kutokuelewana, machafuko na misukosuko!.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...