Mtangazaji nguli wa BBC Charles Hilary (shoto) akisalimiana na beki mkali wa enzi hizo wa Simba SC Shaaban Baraza aliyekuwa mmoja wa wachezaji nyota wa Klabu hicho cha Mtaa wa Msimbazi. Wengi wanasema hajapata kutokea mtangazaji mpira kama Charles Hilary aliyejijengea umaarufu mkubwa enzi za RTD na hadi sasa anapotangaza ligi ya Uingereza. Na wengine wanasema hivyo hivyo kwa uchezaji wa Shaaban Baraza ambaye sasa amestaafu. Wenye data zaidi msaada tutani tafadhali...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Kabla ya Charles Hillary, kulikuwepo akina Salim Seif Mkamba ambae kwa mtazamo wangu alikuwa ndie nguli original wa utangazaji n the best ever....

    ReplyDelete
  2. Seif Mkamba alikuwa mzuri wa mazungumzo baada ya habari sio mpira... Charles yuko juu na ha-boi hata kidogo anakufanya upende kuendelea kusikiliza mpira kutokana na vinjo vyake.

    ReplyDelete
  3. Jamani kwanini tutafute wa kwanza na wa mwisho? Izi tabia za kiupinzani wa kijinga zinatoka wapi. Ukweli ni kwamba Chalz Hillary, Ahmed Jongo na hata mwana mama mmoja nimemsahau wote walikuwa watangazaji wazuri sana. Tuwaenzi sio kuwapambanisha. Maisha sio lazima yawe kuhusu NANI ZAIDI

    ReplyDelete
  4. SekioniKitojo,S.Mbonde,A.Kipozi,mwingine alikuwa mwanza enzi za Pamba(marehemu) nimemsahau jina..RTD hoyeee

    David V

    ReplyDelete
  5. Duu kiswahili kazi jamani....hapo wamepambanishwa au wamesema alikua anatangaza vizuri mpira?

    ReplyDelete
  6. Halima Kihemba - I think she is still alive somewhere dada halima hebu tu - beep basi kwenye blog - upoooo!

    ReplyDelete
  7. WASAALAM MALEIKUM WASIKILIZAJI WETU POPOTE PALE MNAPO TUSIKILZA KWA MARA NYINGINE TENA TUKO HAPA KUWALETEA MATANGAZO YA FINALI ZA KOMBE LA KARUME(KLABU BINGWA)KATI YANGA NA SIMBA.WATANGAZAJI WENU HAPA ABDUL MASUDI BIN JAWEWA AKISHIRIKIANA NA SULEIMAN KUMCHAYA.(YANGA)ELIAS MICHAEL,ATHUMANI KILAMBO,BOI IDDI,HASSAN GOBOSI OMARI KAPERA,ABRAHAMANI JUMA,LEONARD CHITETE,SUNDAY MANARA,KITWANA MANARA,MAULID DILUNGA MOSHY DAYAN.(SIMBA)MAMBOSASA,SHABANI BARAZA,MOHAMEDI KAJOLE,ATHUMANI JUMA,ALOO MWITU,KHALIDI ABEIDI,WILLY MWAIJIBE,HAIDARI ABEID,JMANNE MASIMENTI,ABDALLA KIBADENI,ABASI DILUNGA. THOSE DAYS CHARLES HILARY MZEE WA CHARLANGA YUKO KINONDONI MUSLIM FORM TWO BUT BRATHER CHARLES KATIKA GENERATION YAKE ALIKUWA MKALI NO DOUGHT.

    ReplyDelete
  8. fiyucha ya pleyazi wetu bado si nzuri. utakuta kama huyu maisha yake ya chini sana. mi na adivaisi sana edukesheni sababu wengi inglishi hawajui kwa hiyo inakuwa difikati kwao kutoka na kucheza kwenye nchi zilizo developu. wenye mnaona mzee wa macharanga kichatoka ivo

    ReplyDelete
  9. Nakumbuka enzi hizo za miaka ya tisini charles Hilary alipokuwa akitangaza mpira wa ligi kuu ya Zanzibar kati ya vilabu hasimu kubwa wakati huo Small Simba na Malindi SC katika kiwanja cha Amani mjini Zanzinar. Aliwahi kukiri kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza maishani kutangazia mpira live usiku. kwani ligi ile wakati ule ilikuwa ikichezeshwa usiku.

    Sinashaka yakwamba unguli wa kutangazia mpira ligi za uengereza live kupitia BBC kwake yeye alizipatia hapo Amani

    ReplyDelete
  10. Jamani kwenye kutangaza hamna aliyekuwa anatangaza vizuri,kutangaza vizuri ni sauti yako tu,maana unasema kile unachokiona uwanjani hata wewe unatangaza vizuri ili mradi usiwe bubu tu.
    Sema tu wengi mlikuwa mnasikiliza redio kipindi hicho na TV hamna ndiyo maana mnasema walikuwa wanatangaza vizuri,lkn ukweli ni kwamba kutangaza si kipaji ni sauti hata wewe unaweza.

    ReplyDelete
  11. bila kumsahau Danstan Tido Mhando alietangaza mechi ya kufuzu kucheza kombe la Africa..nakumbuka akisema tunakwenda Lagos...ni ndio ilikuwa mara ya kwanza na mwisho kuiona Taifa stars kufuzu kombe la Africa

    ReplyDelete
  12. Mdau ulie anza na Duu babkubwa endeleza Lugha kwani kiswahili kweli kina kazi

    ReplyDelete
  13. Suleiman Hega na marehemu Abdul Baker ndio waliokuwa wasomaji wa mazungumzo baada ya habari.
    S S Mkamba alikuwa maarufu kwa kuanzisha catch phrase ya duhhhh "ameotea" au "kaotea" ikimaanisha off side!

    ReplyDelete
  14. Siyo Mkamba ni NKAMBA, Salim Seif NKAMBA ambaye sasa ni marehemu. Huyu sikumbuki kama aliwahi kutangaza mpira. Kuhusu mdau aliyeuliza jina la mtangazaji aliyekuwa Mwanza, huyo alikuwa ni Chilambo Dominic. Na huyo mwanamama ambaye mdau amesahau jina lake ni Halima Mchuka.

    ReplyDelete
  15. Nyie wote mnacheza,mtu aliyekuwa anatangaza mpira kwa kusisismua alikuwa mtu mmoja wa kuitwa Ahmed Jongo,kama mnakumbuka ndiye aliyeleta msemo ule wa maguu kumi na mbili ya mtu mzima,alikuwa anamanisha ni penalty na mtu alikuwa akiumia kichogoni alikuwa akisema ameumia kwenye sehemu ya medula oblengata.Kama nitakuwa nimekosea lakini mtakuwa mmenielewa.Na jina langu siweki msije kuniponda bule

    ReplyDelete
  16. Mdau uliyeuliza mtangazaji wa Mwanza ambae sasa ni marehemu ni Nadhili Mayoka na siyo Dominc chilambo kama mdau mwingine alivyosema hapo juu.

    ReplyDelete
  17. ...........Jamani jamani kina baba tafadharini saaaana msilete sharubu zenu kwenye kipindi hiki. kipindi hiki ni cha kina mama tu! KIJARUBA OOYEE!!!

    Abdalah Mlawa bwana, alikuwa moto wa kuota umevaa suti ya mbao.

    ReplyDelete
  18. Pi, pi, pi, pi, pi, pi, pi, pi, sasa hivi ni saa mbili kamili. Na hii ni taarifa ya habari toka Radio Tanzania Dar es Salaam. Msomaji JACOBO TESHA.

    ReplyDelete
  19. Hii ni sauti ya Dar es Salaam msomaji ni David Wakati.........................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...