Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ua kuwasili katika
uwanja wa ndege wa kimataifa was Abeid Amani Karume Air Port,akitokea
nchi za UAE,katika ziara za kuimarisha uhusiano wa kihistoria na nchi
hizo. Picha na Othman Maulid Habari naMaelezo Zanzibar
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar ina mpango wa kufukia eneo la Bahari kwa lengo
la kuongeza Ardhi kwa ajili ya makaazi ili kupunguza ujenzi katika
maeneo ya kilimo.
Hayo
yameelezwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohammed Shein wakatia akizungumza na Waandishi wa Habari hapo
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar mara baada
ya kurejea ziara yake katika nchi za Falme za kiarabu
Amesema
Sharjah imeshafanya kazi hiyo kwa ufanisi na kufanikiwa kujenga nyumba
za makaazi katika maeneo ambayo yalikuwa ya bahari hapo awali.
Aidha
amesema Nchi kama Uholanzi na nyigi nyenginezo zimeshafukia bahari na
kujengwa miji ya kisasa kabisa bila ya tatizo lolote.
Hivyo
alisema Zanzibar inayo maeneo ambayo yakifukiwa yataweza kujengwa
nyumba nyingi za maendeleo kwani miaka ya nyuma kazi hiyo ilifanywa
katika maeneo ya Funguni hadi Makumbusho ambalo eneo lote hilo lilikuwa
Bahari.
Akizungumzia
suala Uwekezaji Dk Shein alisema wakati umefika kwa Zanzibar kupata
maendeleo ya haraka kwa kukaribisha wawekezaji wa uhakika katika Nyanja
mbali mbali ili kuweza kuongeza pato la taifa.
Amesema
kuwa katika mazungumzo yake na viongozi wa Sharjah na Ras Al khaima
wameonyesh hamu ya kuendeleza maeneo hayo ili yaweze kuchangia katika
uchumi wa Zanzibar.
Kuhusu
suala la Maji safi na salama amesema Serikali ya Sharjah italeta
wataalaam wa kuangalia vianzio vipya vya maji kwani utafiti uliofanywa
umeonyesha kwamba maji katika visiwa vya Zanzibar yamepungua hivyo ipo
haja ya kutafuta vianzio vipya kuweza kukabiliana na tatizo hilo.
Akizungumzia
juu ya mafunzo kwa vijana wa Zanzibar Dk. Shein amesema kuwa Sharjah na
Ras Al khaima wamekubali kuwapokea vijana wa zanzibar katika Vyuo vyao
mbalimbali ikiwemo masomo ya Udaktari.
Amewaomba
Viongozi wa Chuo kikuu cha Sharjah kuja Zanzibar kutembelea Chuo Kikuu
cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ili kuona nyanja gani za mafunzo ambazo
wataweza kushirikiana.
watoto hao mbona wamevaa hivyoo jamaniii , ukikutwa umevaa hivi zenji watakuona hufai weye, ila kupokea rais pooaaaaaaaaaaa.
ReplyDeleteUzungu huuuuu mmeona hawatapendeza wakivaa juba hahahhhahahahahahah
kazi ikooooo tena haswaaaaaaaaaaaa
Allah tunusuru
tangu lini watoto wa kizanzibar wanavaa hivyo. Mnatutusi jamani.
ReplyDeleteHAO NI FREE MASON WESHAINGIA HADI Z'BAR.WATOTO WANAFUNDISHWA KUANZA KUONESHA KWAPA NA MABEGA YAO HADHARANI. WAKISHAKUWA WAKUBWA HAWATAONA AIBU TENA MBELE YA WATU.kWELI ALLAH ATUNUSURU NA UZUNGU HUU
ReplyDeleteMhhh jamani, John akiwazuia watoto wa kiislamu kuvaa hijabu, waislaam watakuja juu ile mbaya, lakini mzazi yu radhi kumvisha kama hawa watoto simply because anaenda mpokea Mheshimiwa Rais. Mungu hebu turehemu kwa hili
ReplyDeletekuiga kwing matokeo yake mnashindwa kuwastiri watoto wetu,wangevaa hijab isingependeza???
ReplyDeleteWatoto wa Zanzibar dotcom hao Msiumize vichwa jamni.
ReplyDeleteInatia moyo kwa kila tusikiapo, lamuhimu positive impact kama tutarajiavyo. lakini hapa hatukupata ni nyanja zipi hao wawekezaji wa Sharja na Ras al khaima wamekusudia kuwekeza ili kuchangia uchumi.
ReplyDeleteNakama ni ufukiaji wa bahari basi nilazima tujezingati environmental impact yake kwa maeneo hayo kwamfano:( losses to ecosystems and threatening the thriving existence of fish stocks) na sio kigezo tu eti Zanzibar iliwahi kufukia bahari kutoka funguni hadi makumbusho mnazimmoja ambayo ilikua ni mto tu unaogawa stontown na n'gambo ambao haukua natija sana.
kwa maoni yangu zanzibar bado haijawa na uhaba wa kupelekea kufukia bahari, ila alternative ways zipo kwa mfano kuweka sheria na mipango madhubuti yenye kutekelezeka ili kuondosha ujenzi katika ardhi za kilimo na kuanzisha miradi ya ujenzi itakayotekelezwa na hao wawekezaji na serikali kwa pamoja na sio kuwapa watu viwanja eti wajenge wenyewe ambayo si njia muafaka. ukiangalia viwanja vyengine vipo semu za kilimao ambazo serikali yenyewe imetoa.
Hivi haya mambo yakupokea kiongozi akirudi kutoka ziarani yataisha lini? hawa watu wote waliokuja hapo airport wametumia magari ambayo yanalipiwa na kodi za wananchi, na huko makazini walikotoka si wangebaki tu waendelee na kazi kuliko kuenda kumpokea kiongozi? Hizi siasa inabidi ziishe na viongozi wataongea na simu au video conference kama kuna lolote la kuambiana.
ReplyDeleteNi vibaya sana kuona mavazi ni kila kitu, ni wangapi wanavaa hijabu sana ila wako na waume za wenzao chumba kimoja na halafu ukija mfungo wa ramadhani nao wanafunga? Tunao huku tena waswali sala 5 au 7 kama zipo, msitudanganye uislamu ni roho na si mavazi ndo maana nchi za kiislamu wanapigana kila kukicha wakiamini physical than spiritual. Ankal usibibabie please niachia hii tu
ReplyDeleteWadau naombeni kuuliza,hivi ndege anayotumia Mhe .Shein ndiyo anayotumia Mhe Kikwete?au Rais Zamzibara ana ndege yake na Rais Tanzania ana ndege yake pia?naombeni kujuzwa.
ReplyDeletehali halisi ya tanzania ni kujikwamua kutoka kwenye umaskini kupitia wawekezaji, dah watanzania hatuwezi kufikiria njia nyingine zaidi ya hiyo, anyway haiwezekani labda miaka 2000 ijayo.sasa bahari ikishafukiwa tumaini la masikini kunufakia hipo ama ndo sera za wawekezaji lazma twende kwa njia ya "win win situation"; ila kwa Tanzania mara nyingi huwa ni "win lose situation"..
ReplyDeleteMdau wa 4:15, kosa moja halimaanishi kwamba umeruhusiwa kufanya na la pili.
ReplyDeleteKuvaa wavae vizuri hiyo ndiyo hatua ya mwanzo, ya pili ndiyo wajirekebishe na hayo mengine.