Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na taifa kupitia kwa mamia ya Wazee wa jiji la Dar es salaam katika ukumbi wa PTA jana jioni ambapo alitumia fursa hiyo kuelezea hali ya uchumi wa nchi pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya mchakato wa kupata katiba mpya na kuelimisha  umma nini kinaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Bahati mbaya mheshimiwa hakutaka kuongelea hili swala la kuhofia kuwaudhi wazanzibari wakati wao wanaendelea kutuudhi kwa kauli na vitendo. Kukwepa tatizo sio kutatua tatizo. Tatizo hili lipo na linaendelea kukua kwa kasi. wasilipuuze.

    ReplyDelete
  2. Lini mkubwa ataongea na vijana??

    ReplyDelete
  3. JK jitihada unazofanya lazima tuta zijutia nimeona comments za watu wenye sura za hasira hadi inaudhi ina kua kama vile unapigia mbuzi gita acheze sasa ngoja wanataka moto uwake je?kuuzima wana weza

    ReplyDelete
  4. Munaudhiwa nini, kuambiwa na nyinyi mutetee serikali ya Tanganyika irudi?

    Ha ha hahaaaaaa

    ReplyDelete
  5. uliyetoa maono mwanzo hapo wazanzibari wamekuudhi nini?? acha chuki za kijinga.

    ReplyDelete
  6. Urais kazi kweli kweli."....hupakimbilii....unapakimbilia kwenda kutafuta nini".....??

    David V

    ReplyDelete
  7. hivi wazee wa Dar ndo wawakilishi wa Taifa? maana Presidaa akiwa na issue anaongea nao sijui uwakilishi wa wazee wa mikoa mingine ukoje. Am just trying to think loudly

    ReplyDelete
  8. Jamani mimi ni CHADEMA halisi ila nasema hivi hotuba aliyotoa Muheshimiwa jana mimi naipa 100%, kaongea vizuri sana JK kafafanua yote kwa kina kabisa na kwahilo mimi namshukuru sana. JK ni mwalimu wa walimu,yaani kinachotokea sasa naamini kabisa WAPINZANIA walikuwa na nia ya kupotosha UMMA na mimi walishanilisha sumu hiyo ingawa ni mwenzao, ukweli tushaujua iliyobaki wananchi wenzangu tujenge nchi yetu.Vijenmbe visiishe maana navyo ni chachu katika kuleta mabadiliko na maendeleo ya nchi na watanzania wote kwa jumla.Tuheshimiane, tupendane na tusaidiane. Ila maoni yangu kwa mkuu wa nchi kama ataweza abadilike kidogo awe mkali maana upole KIKWETE umemzidi jamani ndio maana sie chadema tunamchezea ka vile babu yetu. PEACE AND LOVE kwa watanzania wote popote pale mlipo. VIVA TANZANIA VIVA..........ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete
  9. nchi hii chadema watatuharibia...najuwa wachaga wengi na upande fulani wa dini watachonga muda si mrefu...

    ReplyDelete
  10. Faida iliyobaki kwa wazee ni kupiga kura tu, wengi wao wamesha stahafu na asilimia kubwa maisha yao miaka 50 iliyopita ni yale yale! sidhani kama hata kama wanaelewa maana ya credit crunch ni nini kwani wazee hawa hawategemei aina yoyote ya mafao toka serikalini, hawana pension wala social security benefit kwani asilimia kubwa hawakupata bahati ya kuwa watumishi wa serikali na makampuni binafsi. Badala ya kuongea na taifa anaongea na wazee specific wa mji wa Dar! Hapo ni inaonekana alikuwa anatafuta njia ya kufikisha ujumbe wake kuhusiana na maswala ya katiba na power aliyonayo katika kuunda katiba mpya. Ila speech yake ya mambo ya uchumi inajirudia hakuna jipya hapo. NAona bado mheshimiwa anaendeleza siasa za kisanii wakati kuna mambo serious ya kuzungumzia hapa. Next time aitishe mkutano na aongee na vijana kwani ndo viongozi wa taifa la kesho. Mimi nikiwa rais wa nchi nitakuwa ninaongea na taifa sio kikundi fulani tu cha watu. Hakuna jipya na wala la kusisimua katika speech aliyoitoa mheshimiwa ni usanii mtupu bado, hakuna suluhisho ya matatizo yanayoendelea nchini. Mandika yanasema tusiwe wapole kupita kiasi!

    ReplyDelete
  11. wazee wa dar ndio waliompokea nyerere na kumpa nafasi ya kuwa kiongozi wa tanzania hao ndio wazee wa mjini leo hii wazee haohao serikali imewasahau kabisa
    zaidi anakumbukwa nyerere tu
    kina bibi titi wamesahauliwa na wengineo.

    ReplyDelete
  12. Kaongea na wazee Dar lakini ujumbe umefika kwa wazee na vijana wa nchi nzima.Hana uwezo wa kujigawa na kuhutubia kila kona.Chadema hawana utaifa wa kuongoza nchi kitaifa ila wanataka kuichukua nchi kimabavu na waongoze kiubaguzi.

    ReplyDelete
  13. enzi ya baba wenu wa taifa ilikuwa hivihivi..ni wazee wa dar tu walimpa kila kitu leo tumepata uhuru mnajifanya mnajajuwa kila kitu..wakati wazee wakiutaka uhuru mlikuwa mmewakumbatia wajerumani..ipo siku nchi hii kitanuka tuu...tunataka historia ya kweli ya nchi hii..mambo ya kumuona nyerere mungu mtu hatuyataki....ndio maana CHADEMA walikwenda kuungama dhambi zao kwa baba wao wa taifa.....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...