Muda mfupi uliopita, takriban nusu saa sasa, Rais Jakaya Kikwete amemaliza "mazungumzo na Wazee wa Dar es Salaam", mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa PTA jioni ya siku ya Ijumaa ya 18 ya mwezi Novemba 2011.

Rais "alizungumzia" kuhusu "Hali ya Uchumi nchini" pamoja na "Mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya".

Ifuatayo ni audio yenye sehemu ya "mazungumzo" hayo.

Audio hii ina urefu wa saa 1 na dk 6.

Haikuwezekana kurekodi tokea mwanzo kutokana na sababu  zilizo nje ya uwezo wangu kutokana na kuwa na majukumu ambayo hayakuniwezesha kuipata sehemu ya mwanzo. Pengine wapo waliorekodi sehemu nzima ya "mazungumzo" na tutumai wataipakia mtandaoni ili upate kuisikiliza tokea mwanzo.

 http://www.wavuti.com/4/post/2011/11/mazungumzo-ya-rais-kikwete-na-wazee-wa-dar-es-salaam-18-11-2011.html#ixzz1e5RsZxHv

 Baadhi ya wazee wa Dar es salaam wakifurahia baada ya Rais Kikwete kumaliza kuongea nao leo ukumbi wa PTA jijijni Dar. Juu hapo  kuna link ya sehemu ya hotuba hiyo toka kwa Da'Subi
Rais Kikwete akiondoka kwa furaha baada ya kuhutubia wazee wa jiji la Dar es salaam jioni hii. KUPATA HOTUBA HII BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. who are these Dar es Salaam wazee?. WHAT KIND OF STRUCTURE DO THEY FORM IN THE REPRESENTATION. Hii kitu yachanganya sana mimi.

    ReplyDelete
  2. Nimeipenda hotuba ya Mhe Rais JK KIKWETE, ameongea kwa upole na facts.

    ReplyDelete
  3. Wewe unayechanagnyikiwa na structure ya wazee wa darisalama, kwani wewe ulipokuja darisalama hukuwakuta wenyeji? au unadhania kila mtu hapa darisalama ni wakuja kama wewe?
    Kwa taarifa yako structure hii ndiyo ile ile iliyomwambia nyerere kwamba "aaah...! hapa watu wazima hatuvai kaptula yakhe, tutakufundisha kuvaa suruali". Na walipotaka kumtahiri akakimbilia kanisani, wazungu wakamtetea kwamba kama mtu hataki kutahiriwa asilazimishwe.

    ReplyDelete
  4. Ina maana wazee wa Dar es Salaam ni waislamu tu?

    ReplyDelete
  5. Anony wa sat. Nov 19 1:00 2011

    Kichwa chako kimejaa ile kitu sisi nyumbani tunaita MASHI (feces)

    ReplyDelete
  6. Hapa Raisi ndipo anapochanganya mambo, ni kheri angekaa na kuhutubia taifa kwa ujumla kuliko hao wazee wa dar es salaam. asisahau kwamba Nchi si ya watu wa dar es salaam peke yao ni ya watanzani wote na matatizo yanayotokea yanahusu Tanzania nzima na si hao wazee peke yao. Mbona anachanganya mambo kila kukicha ni kheri angesomba wazee kila mkoa na si mkoa mmoja tu

    ReplyDelete
  7. alihutubia wazee wa kiislam kama inavyoonekana kwenye picha full stop!!

    ReplyDelete
  8. Lakini SI UJUMBE WATANZANIA WOTE TUMEUPATA? Rais kuhutubia taifa kwa kupitia mikutano ni JADI YETU WATANZANIA.. Jana haikuwa mara ya kwanza na wala haitakuwa ya mwisho Rais kutumia 'FOCUS GROUPS' kufafanua jambo na kuelemisha watanzania. Mimi hapa London nimeisikiliza hotuba yote mwanzo hadi mwisho - In fact I did like it as it was 'evidence-based' Big-up guys!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. wewe unayesema nyerere kutahiriwa wakati anakuja dsm nyerere alikuwa tiyari kaisha tahiriwa maana wao kwao mpaka wanawake wanawatahiri

    ReplyDelete
  10. wakristo kubalini dar waisilamu wako wengi hizo ni chuki zenu kuona kanzu na kofia hilo ni vazi acheni ushamba mnataka wakakusanywe wakulima waje kuhutubiwa dar hamjui maana ya mtandao lakini ujumbe umefika

    ReplyDelete
  11. Nyie mnaochanganyikiwa na wazee wa darisalama, hata sisi pia mnatuchanganya sana mnapojiita eti nanyi pia ni washabiki wa Yanga au Simba wakati babu zenu hawakucheza tokomile Mbango na Mizia. Usiniulize Mbango na Mizia ndiyo kitu gani. Kama hujui Mbango na Mizia basi wewe siyo Yanga na wala siyo Simba isipokuwa unajipendekeza tuu kama mnavyojiita manchester united na liverpool.

    ReplyDelete
  12. Wewe anonymous wa 8:37, hao wazee si ndiyo wenye mji huu wa Mzizima? Wengine wa migolole ni wa kuja tu.

    ReplyDelete
  13. WEE MDAU WA 3.54 HIVI HUJUI HISTORIA YA DAR?HIVI HUJUI MKOA HUU WATU WAKE WA ASILI NI NANI?PAMBAFU KABISA!!!!MM HUU MKUTANO UNGELIFANYIKA MUSOMA AU MOSHI NA MAJORITY YA WATU WAKAWA NI WAKRISTO BASI LISINGE NISHANGAZA MAANA NDIO FACT. NA UNA UHAKIKA GANI KUWA WATU WOTE WA HUMO NI WAISLAM? ACHA ZAKO WW, PUNGUZA JAZBA.

    ReplyDelete
  14. Hata huyo Nyerere mara kibao alikuwa akiongea na "wazee wa Mzizima, na baadae Dar es Salaam". Alipokuja Mwinyi na yeye aliendeleza utaratibu huo huo na hata Mkapa nae alikuwa akikutana na kuongea nao.

    Sasa nyie msioheshimu wazee tutawaona ujanja wenu! Mnafikiri kila kitu ni dot com tu.

    ReplyDelete
  15. Anonymous wa 4 wa 6 na wa 7 kutoka juu.

    AVOID RELIGIOUS SENTIMENTS!!!...
    yaani kugawa watu kwa misingi ya UDINI!!!

    Mkae mkijua kuwa hata ktk nchi za Ughaibuni mfano MAREKANI bila NEW YORK CITY inakuwa hapatoshi, na UK bila LONDON inakuwa hapatoshi.
    Mmeshuhudia Gaddafi wa Libya alipoiachia TRIPOLI ndio ukawa mwanzo wa kuanguka kwake.

    Hapa sasa ndio tatizo lenu linapoanzia, ndio ninyi mnaobeza structure group /focus groups na KUDHARAU MCHANGO WA WAZEE WA DAR ES SALAAM KTK UHURU,SIASA NA TAIFA,,,,WAKATI MUHIMILI WA KILA TAWALA YA NCHI YEYOTE NI MJI MKUU AU MKONGWE NA WAKAZI WAKE WAKONGWE....JE KAMA ALIKUSUDIA KUWAHUTUBIA WAZEE WA DINI MOJA NDIO HIVYO ALIVYOTANGAZA? AU KUWAALIKA?, AU MNA UHAKIKA GANI KAMA KTK WALIOHUDHURIA WA DINI ZINGINE HAWAMO?....mara nyingi mkiambiwa Wazee wana influence ktk nchi yeyote mnabisha na mnaleta udini....SASA NINI?

    ReplyDelete
  16. WEWE WA 4, WA 6 NA WA 7 KUTOKA JUU ACHENI MITAZAMO YA UCHOCHEZI!!!!!!

    Kwani Raisi au Ikilu ilitoa tangazo kuwaalika Wazee wa Kiislamu tu wa Dar Es Salaam?

    Kwani ni mara ya kwanza Raisi wa sasa kuongea na wazee wa Dar?

    Pana awamu nne za maraisi hadi sasa, 2 Wakristo Nyerere na Mpaka na 2 Waislam Mwinyi na Kikwete na ktk vipindi vyote hivyo marais wamekuwa wakiongea na wazee wa Dar Es Salaam mara kwa mara,kuna ajabu gani?

    Je ktk hao maraisi waliopita kuna Raisi aliyewahi kutoa tangazo la kuwaalika wazee wa Dar Es Salaam ambao ni Waislamu tu na kuwabagua wengine?

    Mna uhakika gani kuwa hao wote pale waalikwa ni Waislamu tu? ..mlipewa daftari la mahudhurio mkahakiki kuthibitisha?

    Acheni tathmini finyu za kuangalia muonekano tu wa picha ya wahudhuriaji!

    TOENI MAONI ENDELEVU NA SIO UCHOCHEZI NA KUASHIRIA MGAWANYIKO NA UBAGUZI WA KIDINI!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Kwasababu amehutubia wazee Dar ndio maana mkaona kanzu nyingi.Kwani hamjui kama wenyeji wa Dar asilimia kubwa ni waisilamu na wakristo ni wakuja tu?Au kwasababu mmevamia jiji la wazaramo na kuuza ardhi yote kwa wagalatia na kujenga makanisa.Hii ni DAR ES SALAAM na nyinyi mnayo mikoa yenu yenye asilimia kubwa ya ukristo.Na siku akienda mikoa fulani basi na nyinyi mtafurahi kwa sababu mtaona misalaba itakavo pamba moto.

    ReplyDelete
  18. "nyerere alikuwa tiyari kaisha tahiriwa "

    Nyerere hakuwahi kutahiriwa.

    Mtu kama huyu naye anajifanya hajui kama Darisalama ni ya waswahili. Angalia kiswahili chake kwanza.

    ReplyDelete
  19. Ndugu yangu unauliza samaki Feri au Pwani?
    ___________________________________

    NDIO WAZEE WA DAR ES SALAAM NI WAISLAMU;
    ___________________________________

    WAO NDIO WALIOANZISHA CHAMA NA NDIO MSINGI WA NCHI NA UHURU UNAOJIVUNIA WEWE , HATA HIYO PICHA UNAIONA WENGI WAO NI NANI?

    ReplyDelete
  20. 1.Dar Es Salaam=UISLAAM,

    2.Dar Es Kristo=Ukristo,

    SASA HAPO JUU 1. au 2. IPI IMEKAA SAWA?

    ___________________________________
    ITAWAUMA BAADHI YENU ILA TUACHE UBISHI USIOKUWA NA MANTIKI!!
    ___________________________________

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...