Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo akiwasili Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo akifuatana na Mkuugenzi wa  Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Paul Msemwa, katika kukagua mradi wa Makumbusho hiyo.
 Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo akipata maelezo toka kwa muhihadhi wa Mila na Desturi Bw Achiles Bufure wa  Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
 Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo  akiendelea na Ukaguzi wa Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
 Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo akikagua Ukumbi wa kisasa wa maonesho ya jukwaani wa  Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
Katibu mkuu Kiongozi Bw Philemon Luhanjo akishauri jambo baada ya kuangalia nyumba ya Kabila la Wabena iliyopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam

Na Sixmund J. Begashe

Katibu mkuu kingozi Bw PHILEMON LUHANJO ameushauri uongozi wa makumbusho ya Taifa kuboresha Mahusiano yaliyopo kati yake na wafadhili hasa wale wakimataifa, kwakuwa nimuhimu katika kuimarisha Mashirikiano yaliyopo kwa maslai ya nchi yetu.

Bw Luhanjo amesema kuwa kujenga mahusiano mema na marafiki wa nje haiitaji garama bali ni ukaribu nao na kuyajali mahusiano hayo na si kuyapuuza kwani hata mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni umetokana na Mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Tanzania nay a Sweden. Katibu mkuu Kiongozi alisema siyo vyema kwa watumishi kulumbana katika jambo ambalo ni lamaendeleo ya taifa letu.

Bwana LUHANJO aliwapongeza wahisani wa nchini Norway ikiwemo Progaram ya kiswidishi ya ICT katika nchi zinazo endelea inayo ratibiwa na Idara ya Komputa ya Chuo kikuu cha Stockholm Sweden (Spider) kwa kuufadhili mradi wa makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam ambapo ilitoa Milioni 120 kwa ajili ya manunuzi ya Computer za Maktaba na Vifaa vya kurekodia kumbukumbu kwa njia ya sauti na video.

Hatahivyo Bwana LUHANJO aliupongeza Uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kuusimamia vyema mradi wa Makumbusho hiyo na kusema kuwa ni moja kati ya miradi mikubwa ambayo serikali inapaswa kujivunia kama sehemu ya sherehe za Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Uhuru wa Nchi yetu.

Pamoja na kumshukuru Kataibu Mkuu Kiongozi kwa kutembelea Mradi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Dkt Paul Msemwa alisema kuwa wanakabiliwa na changhamoto kama vile Uchache wa wafanyakazi na uhaba wa vitendea kazi.

Akiutembela Maradi huu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bwana LUHANJO alijionea sehemu mbalimbali kamavile Ofisi, Chumba Mahususi kwa Mikusanyo nyeti, Bohari za mikusanyo, Kumbi za Monesho, Seheumu za watoto za kujifunzia kazi mbali mbali za sanaa, Ukumbi wa kisasa wa sanaa za maonesho ya Jukwaani, Studio ya Kurekodia Musiki, Maktaba ya Kisasa, Kumbi za Mikutano na Sherehe mbali mbali, Duka la Zawadi ,Mgahawa na Viwanja vya wazi kwa ajili ya Shughuli mbali mbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...