Mratibu wa Kinga ya Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Peres Kamugisha (kulia) akipokea mwenge kutoka kwa mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa mwaka huu,Elisha Lawrence Gama,mara baada ya kuwasili wilayani humo hivi karibuni.
Mkimbiza Mwenge kitaifa mwana huu,Elisha Lawrence Gama akitoa ujumbe wa mwenge kwa wananchi wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma katika viwanja vya CCM wilayani humo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akijiandaa kumpa tone la vitamini A mtoto wa miaka 2 Athumani Idd baada ya kuzindua zoezi la chanjo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wilayani Namtumbo hivi karibuni.
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa,Bi Mtumwa Rashid Alfani akimpatia tone la vitamini A mtoto Suzy Lucas Njela ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa zoezi la chanjo kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hivi karibuni,ambapo Wilaya hiyo imekusudia kutoa chanjo ya magonjwa mbalimbali kwa watoto zaidi ya 143,133 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na wilaya zingine za mkoa huo.Picha na Muhidini Amri wa Globu ya Jamii - Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwenge huo mwenge...mbio mbio...Umulike vijijini....mbio mbio.Ilikuwa burudani kweli enzi za mwlm.

    David V

    ReplyDelete
  2. Elishaaaa-nakuona mwana umekuwa mzalendo wa ukweli. Poa sana.

    Vijana wako wa Chemba ya Muungano, Mazengo Complex tunakukubali.

    ReplyDelete
  3. MIAKA 50 YA UHURU::::TUMETHUBUTU, TUMEWEZA NA TUNASONGA MBELE!!!!!
    -----------------------------------
    Pana umuhimu tuutumie MWENGE WA UHURU kimaslahi endelevu, kwa kuwachoma MAFISADI NA MOTO WAKE ifikapo ktk sherehe za kumaliza mbio za mwenge tena shughuli hii iwe hadharani kama ktk Uwanja mpya wa Taifa, ili kumuenzi BABA WA TAIFA KAMBARAGE NYERERE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...