Mkuu wa Wilaya ya Arusha akimkabidhi Meya wa Arusha Mstahiki Gaudence Lyimo vifaa vya usafi kutoka TDL.
Kinywaji cha KONYAGI kinachozalishwa na kampuni ya TANZANIA DISTILLERIES LIMITED (TDL) kimetimiza miaka arobaini (40) tangu kuanza kuzalisha mnamo mwezi Oktoba 1971.
Katika kusheherekea miaka 40 ya mafanikio ya kinywaji hicho na kampuni ya TDL kwa ujumla, TDL imetoa misaada ya vifaa vya usafi kwa jiji la Arusha. Vifaa hivi vya usafi vimekabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh. Raimond Mushi pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mh. Gaudence Lyimo.
Kama Mkurugenzi wa TDL alivyoahidi wiki moja iliyopita alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 40 ,Konyagi itaanza na Arusha kwa vifaa vya usafi kwa manispaa ya Jiji. Vifaa hivyo vinavyotolewa na Konyagi vina thamani ya shilingi milioni kumi (TSh10,000,000).
“Nia ni kuchangia juhudi za kuimarisha usafi katika majiji ya Arusha, Mwanza na Dar es Salaam Ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo ya jamii, TDL itashiriki katika kuhamasisha kampeni za usafi wa mazingira katika kuendeleza usafi na mandhali safi ya majiji yetu.” Alisema Ndugu David Mgwassa.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Matoroli, vest zenye reflectors, gloves, masks, kofia za usalama, miwani ya kuzuia vumbi na jua, gum boots, mifagio, majembe na reki.
Mwanza na Dar es Salaam pia watapata misaada kama hii katika mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 40 ya Konyagi.
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited ilianzishwa mnamo mwaka 1970 tarehe 10 Mwezi Aprili kama mradi wa shirika la Mandeleo la Taifa (NDC) kwa ushirikiano na kampuni ya maendeleo ya kifedha ya TDFL pamoja na kampuni mbili za kimataifa, Duncan, Gilbey’s & Matheson (DGM), International Distilleries and Vinters (IDV) na mfanyabiashara mjasiriamali aliyejulikana kwa jina la Chande.
Dhumuni la kuanzishwa TDL lilikuwa ni kupambana na unywaji wa pombe haramu ya Gongo kwani TDL ilipewa jukumu lakutengeneza kinywaji mbadala kwa Gongo kilicho safi na salama kwa wanywaji.
Mnamo mwaka 1972 kiwanda kilifunguliwa rasmi na kilianza uzalishaji kikiwa na uwezo wa kuzalisha katoni 50,000 kwa mwaka.
Mwishoni mwa 1970, kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ilinunua hisa zote zilizokuwa zikimilikiwa na NDC na hivyo TBL ilipouzwa kwa kampuni ya Bia ya Afrika Kusini (SABI) (kupitia mpango wa serikali ya Tanzania wa ubinafsishaji makampuni ya Umma) SABI ilimiliki pia kampuni ya TDL. Ni wakati huu pia makampuni binafsi ya DGM na nayo yaliuza hisa zake kwenye TDL kwa TBL.
Mnamo mwaka 2004, TBL ilimkaribisha mwekezaji mwingine, DISTELL, kumiliki hisa za TDL kwa asilimia 35. DISTELL ni kampuni iliyobobea katika utengenezaji na uuzaji wa mvinyo na vinywa vikali.
Hata hivyo TDL inaendeshwa kama kampuni huru chini ya usimamizi wa timu ya Utawala wake binafsi yenye jukumu kamili la kuendesha shughuli zake za kila siku na kuhakikisha kuwa TDL inafikia malengo yake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...