MAREHEMU EMILY TIKU GELLEGE
24th May 1948--------29th Nov.1996
Leo mama yangu ni miaka 15 kamili tangu uitwe na MUNGU.
Amani ya MUNGU ipitayo akili zetu na upendo wa MUNGU baba ulio wa ajabu na ahadi zake za kweli, Pengo ulilotuachia kamwe HALIZIBIKI.
Bado tunakukumbuka kwa Upendo,Busara,Wema na Mafunzo uliyokuwa unayatoa katika familia.
Mwanao nilikupenda sana na nilitaka sana kuendelea kuishi nawe kumbe MUNGU alikupenda zaidi. Unakumbukwa sana na mwanao pekee Ruth, mkweo Eugene na wajukuu zako Emily na Ervin. Pia unakumbukwa sana na Wajukuu zako,Watoto zako, Dada zako,Wadogo zako,Kaka zako,Ndugu,Jamaa na Marafiki.
MUNGU aendelee kukupumzisha kwa Amani.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake Lihimidiwe!!!!.
Kwa namna ya pekee siku ya leo tunakukumbuka mama yetu mpendwa , binafsi na wajukuu zako ( emily na ervin ) ambao hatukupata nafasi ya kukuona lakini tunamshukru mungu kwamba tumeendelea kuvuna busara na hekima zako kutoka kwa mwanao wa pekee. Tunaomba mungu andelee kukupumzisha kwa amani.
ReplyDeleteR.I.P Mama mdogo, daima tutakukumbuka kwa upendo, hekima na busara zako.
ReplyDeleteMungu ni mwema
Mazila
Mungu Ampe Pumziko la Milele Aliyetutangulia!!
ReplyDelete