Asalaama Alaykhum wajina
Kwakweli hali bado ni tata sana ya mafuta kwa mji wa mtwara kwa hata kile kituo kimoja cha Gapco kilichokua kina mafuta ya kusubiri kwa foleni ya masaa 8 had 10 nacho sasa kimeishiwa toka juzi usiku na jana yote hapajauzwa mafuta sehemu yeyote halikadhalia leo mji mzima hauna mafuta.
Sasa bei za bajaji, piki piki na taxii zinapanda na wengine kulazimika kupaki kabisa magari yao. Wamejitokeza wachuuzi walifanikiwa kununua mafuta kwa magaloni sasa wanauza mafuta haya kwa shilingi elfu 5000
kwa lita moja nunua hutaki acha watanunua wenye pesa.
Walah tunateseka wenye vyombo vinavyotumia petroli kila mmoja anasema yake ukweli haujajulikana je ni kweli bidhaa hii ni hafifu au kuna mgomo baridi?????
WAHUSIKA WENYE MAMLAKA LIANGALIENI HILI MTUNUSURU YARABI
MDAU MTWARA
Miaka 50 ya "UHURU TUMESUBUTU TUMEWEZA TUNASONGA MBELE + MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA= CCM OYEEE!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMAFUTA...suluhisho lake bado kitendawili!
ReplyDelete