Fundi wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), Issa Mohamed akionyesha simu ya kuzungumsha kwa mkono iliyokuwa ikitumika mwaka 1973 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya sekta ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia yaliyomalizika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mhandisi, Dominick Ngandama na Ofisa Uhusiano wa TTCL, Amanda Luhanga.
Baadhi ya watu waliofika kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ya sekta ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakipata maelezo kutoka kwa Fundi wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), Issa Mohamed.
Simu za Mezani zilizotumika enzi hizo.
Fundi wa TTCL, Issa Mohamedi akionyesha Simu za kisasa.
Mtambo ambao Opereta aliutumia kwa kuunganisha simu za wateja enzi hizo.
Ofisa Mkongo wa Taifa, Thomas Lemunge akionyesha ramani inayoonyesha mikoa iliyounganishwa na mkongo wa taifa.
Ofisa Biashara wa TTCL Adam Issah akitoa maelezo kuhusu huduma wanazozitoa.Picha na Francis Dande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. TTCL kama Tembo...Haina Mwendo...wame provide very bad service na mpaka leo hawana budi ya ku provide good customer service. They should not be at the show....shame on TTCL

    ReplyDelete
  2. nyie TTCL mko juu ,mnaweza lakini urasimu wenu na ufisadi wa ndani na nje ya kampuni unawamaliza.safisheni nyumba yenu mfanye biashara

    ReplyDelete
  3. Mmetutoa mbali sana POSTA/TTCL..wakati niko "sekondari bodingi" nilikuwa naenda kwenye kibanda cha simu POSTA nazungusha hiyo midude kitu kinaitwa 'reverse call' -'opareta' ananiambia subiria..nasubiria...halafu baadae 'opareta' ananipigia hapo hapo kibanda cha simu "haya ongea"..kweli Miaka 5O ya uhuru.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...