Wahadhiri wa chuo cha mipango wakielekea kwenye ukumbi wa mwalimu Nyerere tayari kwa sherehe za mahafali.
Wageni mbalimbali walioshiriki katika mahafali hayo pamoja na uongozi wa chuo
Mkuu wa chuo cha Mipango Dodoma Bw. Costantine Lifurilo akizunguma kwenye mahafali hayo ambapo ameomba wizara kusaidia kukamilisha jengo la ghorofa saba ambalo litapunguza uhaba wa vyumba vya kusomea. Mipango-Alama maalumu ya weredi ya Chuo cha Mipango Kitabu cha Planners Handbook (ambacho ndiyo msingi wa mafunzo ya Mipango ya Maendeleo ya Chuo hicho)
Naibu waziri wa fedha Gregory Teu akimtunuku Mhitimu wa stashahada ya Uzalimi ya Mipango ya Mikoa katika mahafali hayo.
Wahitimu wa Shahada ya Mipango ya mazingira
Wahitimu wa kozi mbalimbali kama mabango yao yanavyoonyesha


Na Mwandishi wetu.

Naibu waziri wa Fedha Mh Gregory Teu ameutaka uongozi wa chuo cha Mipango na Bodi yake kuangalia uwezekano wa kuwaajiri wahitimu wanaofaulu vizuri masomo yao ili kutumia rasilimali zilizoandaliwa chuoni hapo kusaidia wenzao badala ya kusubiri kuajiri kutoka nje.

Ameyazungumza hayo jana jioni kwenye mahafali ya 25 ya chuo cha Mipango Dodoma ambapo alikuwa mgeni rasmi. 

Amesema ni vyema chuo kikaanza kutumia vijana waliofaulu vyema kwenye shahada zao za kwanza kama inavyofanyika kwa vyuo vingine na hatimaye kuwaendeleza kwa ngazi za juu hatua ambayo itasaidia kupunguza pengo la wahadhiri  wasaidizi.



Mapema katika taarifa yake mkuu wa chuo hicho Costantine Lifurilo amesema,chuo hicho ambacho kimeanza mwaka 1979 kikiwa na wanafunzi 22, kimeendelea kukua ambapo hadi kufikia mahafali ya leo kimehitimisha wanafunzi 1477 kiwango ambacho amesema kimesaidia kupunguza pengo la wataalamu wa mipango katika ngazi mbalimbali za serikali na hasa serikali za mitaa.



Amesema pamoja na hatua hizo, chuo kinakabiliwa na tatizo la ukosefu wa miundombinu ya kufundishia na kuiomba wizara kuangalia uwezekano wa kuwezesha ukamilishaji wa jengo la ghorofa saba ambalo litatumika kwaajili ya mihadhara, ofisi na kumbi za kusomea.



Mapema katika salam zake Mwenyekiti wa bodi ya chuo Dr Razack Lokina amesema kwa sehemu kubwa chuo kimeweza kutekeleza malengo yake  ya mpango mkakati unaoishia 2014 na kwamba hatua inayokusudiwa sasa ni kuanzisha shahada mbili za uzamili baada ya kukamilisha kwa miundombinu muhimu ya uendeshaji mafunzo hayo.



Amesema hayo yote yamefikiwa kutokana na ushirikiano baina ya chuo hicho, wizara ya fedha ambamo chuo hicho ni sehemu yake, na baadhi ya wadau wahisani kutoka nje.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Zaidi ya shahada walizotunukiwa wasije tena wakasema...mipango si matumizi!

    ReplyDelete
  2. Hiyo sera ya kusema wanaofanya vizuri waajiriwe na chuo ni fix tu
    Labor market ni function ya demand and supply..simple.

    ReplyDelete
  3. Safi sana nilipenda mavazi yao sijui walinunu wapi?

    ReplyDelete
  4. Safi sana nimependa sana majoo yao sijui walinunua wapi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...