Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya EPZ, Dr A. Meru, pamoja na mwakilishi wa Kampuni ya Lena Holdings and Investment Tanzania ltd Bwana Saleem Sheikh, wakiweka sahihi kwenye Mkataba wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Tehnologia ya Komputa jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya EPZ, Dr A. Meru, akipeana mkono wa pongezi na mwakilishi wa Lena Holdings and Investment Tanzania ltd yenye makao yake makuu huko Dubai mara baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Teknologia ya Komputa (ICT Hub). Mbele kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya usambazaji wa vifaa vya Komputa,DESPEC International Ltd, Bwana Riaz Jamal.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya EPZ, Dr A. Meru, akiongea na Wawekezaji wa Kampuni ya Lena Holdings and Investments Tanzania Ltd, inayokuja kujenga kituo cha kisasa cha Teknologia ya Komputa (ICT Hub). Kituo hiki ni cha kwanza Afrika ya Mashariki na kitatumia mtaji wa zaidi ya Shs. 17 bilioni na kuajiri watu zaidi ya 500.
SASA WEWE MWAANDISHI WA HABARI UMEYAONA WAPI YA KWENDA KUSIMAMA KATIKATI YA HIGH TABLE JUST KWA AJILI YA KUSHIKA HICHO WHATEVER NI KIJIMICROPHONE AU VOICE RECORDER,SI KUTIANA AIBU KATIKA FANI YA ISSA MICHUZI.
ReplyDeleteKuna Matatizo katika reporting ya Habari hasa za Tekinolojia. Kituo cha Tekinolojia ya Kompyuta cha nini? Kitafanya kazi gani na kitatusaidiaje?
ReplyDelete