Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Kepteni Mstaafu , Seif Mpembenwe, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa huo, Luteni Mstaafu Chiku Galawa, Novemba 24, mwaka huu mpakani mwa Mikoa hiyo eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero.
 Kiongozi wa  Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akizundua jengo la mradi wa Benki Mazao katika Kijiji cha Dihinda, Wilaya ya Mvomero , Mkoani Morogoro,  Novemba 24, mwaka huu  wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani hapa.
 Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , ( wapili kutoka kushoto) akiuliza Mkulima, Hamida Mrisho  wa Kilimo cha Umwagiliaji wa zao la Mpunga katika  Kijiji cha Mkindo, Wilayani Mvomero,  Novemba  24, mwaka huu  juu ya uzalishaji wa zao hilo kwa ekari ,wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani hapa,( watatu kushoto) ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa , Halima aDendego , ambaye ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero  na Morogoro.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akisoma hotuba ya Mkoa wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Tanga, eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.
 Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akikaaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, kutoka Mkoa wa Tanga, eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.
Kiongozi  wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2011, Mtumwa Rashid Khalfani , akiagana na viongozi wa Mkoa wa Tanga na kukaribishwa na viongozi wa Morogoro, wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru,  eneo la Kijiji cha Mziha, Wilaya ya Mvomero, Novemba 24, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ukosaji wa kazi kweli ni tatizo kubwa !!!

    ReplyDelete
  2. tutumie nguvu zetu kuondoa matatizo halisi yanayowakumba wananchi,tusijihusishe na mambo ambayo practically hayatatui matatizo tulionayo.Mwenge umekuja mara ngapi?wanaoukimbiza wanapewa allowance kubwa,watoto wanajipamnga barabarani ukiondoka matatizo yao yapo pale pale.

    ReplyDelete
  3. huo ndio uchawi wa kizanaki yaani huo ni muzimu wa mwenge wazaramo wanaita kibwengo,wahaya wanaita kimuri yaani mzimu wa moto hapo hakuna kitu kama mdau alivyosema ni uzembe tu vitu visivyo kuwa na maendereo

    ReplyDelete
  4. Mwenge uwekwe jumba la makumbusho! matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. Maaraba ngapi za shule zingejingwa kwa fedha zinazotumika kuuzungusha mwenge nchi nzima. Hakuna mantiki ya Mwenge wa Uhuru katika karne hii, huu ni ukweli usiopingika.

    ReplyDelete
  5. Ni wakati m uafaka wa kuuweka mwenge kwenye makumbusho ya taifa na kutumia muda tunaopoteza kwa kukimbiza mwenge kutatua matatizo ya nchi.

    ReplyDelete
  6. MWENGE BADO NI MUHIMU SANA::::::::

    Itafaa tukiutumia mwenge kwa njia hizi mbili:

    1.Mafisadi wakamatwe na waumbuliwe hadharani ktk sherehe za kumaliza mbio zake mbele ya wananchi na Raisi,,, huku Mafisadi wakikumbushwa kuwa mfano ktk picha ya Viongozi hapo juu Waasisi wa nchi walijitahidi uadilifu.
    (((Itafaa wajifunze kuwa waadilifu)))

    2.Moto wa mwenge utumike kwa kuwaamuru Mafisadi kuweka viganja vyao na kuchomwa na moto huo ili iwe adhabu kabla mwenge haujazimwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...