Na Francis Godwin
MFANYABIASHARA maarufu mjini Iringa Bw. Bader Saleh Abri amejitolea msaada  wa  pikipiki moja kwa ajili ya kulisaidia  jeshi la polisi  wilaya ya Mufindi mkoani  Iringa ili  kuzidi  kuendeleza kazi  nzuri ya  ulinzi .

Akikabidhi msaada  huo wa  pikipiki moja leo kwa mkuu wa polisi  wilaya ya Mufindi (OCD)Peter  Kakamba, Bw Abri  alisema kuwa  amevutiwa zaidi na utendaji kazi  wa jeshi la  polisi mkoa  wa Iringa na hivyo kuamua  kutoa pongezi  zake kwa  jeshi  hilo kwa  kulisaidia  kitendea kazi kama njia ya kuhamasisha  wafanyabiashara na wananchi wengine  kuendelea kuwa  jirani na jeshi la polisi.

Bw. Abri  alisema kuwa  pamoja na kazi nzuri  inayofanywa na jeshi la polisi mkoa  wa Iringa chini ya kamanda wa polisi  Evarist Mangalla  na ile inayofanywa Tanzania  nzima chini ya mkuu  wa polisi nchini (IGP)  Said Mwema bado  jeshi  hilo linapaswa  kupewa ushirikiano mkubwa na watanzania  wote  wenye mapenzi mema na amani ya Taifa   hili.

Hata  hivyo  alisema kuwa  bado  wafanyabiashara   ndani ya mkoa  wa Iringa  na nje ya mkoa wa Iringa wanapaswa  kuendelea  kujenga ushirikiano  na jeshi la polisi katika maeneo yao huku asisisitiza  kuwa misaada  ya vitendea kazi kwa jeshi la  polisi  isilenge maeneo ya mijini pekee bali ielekezwe  pia maeneo ya vijijni ambako kuna changamoto kubwa .

Kwa upande  wake mkuu  wa Polisi wilaya ya Mufindi (OCD) Kakamba akishukuru kwa niaba ya kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa kwa msaada  huo alisema  kuwa ,msaada  huo ni changamoto kwa  wadau  wengine  kuendelea  kushirikiana na jeshi la polisi kupitia  dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi .

Alisema  kuwa pamoja na kuwa Abri ni mkazi wa Iringa mjini ila ameamua  kutoa msaada  wake wilaya ya Mufindi na kuwa huo ni mfano kwa wadau  wengine  kuendelea  kuinga mfano wa mfanyabiashara  huyo  ambaye anatambua  maana ya ulinzi na usalama  wa Taifa  hili na dhana iliyopo ya polisi jamii na ulinzi  shirikishi pamoja na kauli mbinu ya jeshi la polisi  ya ukamataji bila   kushurutisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mimi iko patia wewe pikipiki alafu iko taka kamata mimi tena.abana bana iko mimi toa saada alafu mimi ikoniachie.
    anyway it is good to see samaritarians helping the police force but the government should be doing this rather than individuals.

    Mkulima Njia Panda Nyololo

    ReplyDelete
  2. wewe mjinga hapo juu huyu sio muhindi ni muarabu, akili zako hazina akili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...