Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Arusha Mjini (CCM),Mhe. Namelo Sokoine akiwasiliana na wanafamilia yake kwa njia ya simu huku akiwa kavalia mavazi ya jamii yao ya kimasai alizozawadiwa na waumini wa Kanisa Katoliki lililopo kwenye kijiji cha Lolera Wilaya ya Kiteto,muda mfupi baada ya ibada kufanyika kanisani hapo.
Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Arusha Mjini (CCM),Mhe. Namelo Sokoine akizungukwa na wakinamama wa jamii ya kimaasai na kusikiliza maelezo ya ujenzi wa kanisa.
Mbunge wa Viti Maalum jimbo la Arusha Mjini (CCM),Mhe. Namelo Sokoine akiongozana na Father Saning'o na baadhi ya wananchi wengi waliofulika kwenye eneo hilo,wakielekea kuingia kwenye ofisi za Kanisa Katoliki kijini hapo kwa ajili ya mgeni wao kusaini kitabu cha wageni.
Safi sana dada..yaani umependeza sana na hao akina Mama.Kama Swaziland vile..
ReplyDeleteDavid V
Jamani hilo jina mmekosea,
ReplyDeleteanaitwa nameloku, means sweety'
Ameolewa? Kama bado tuwasiliane
ReplyDeleteIs she the daughter of the late Edward Moringe Sokoine??
ReplyDeleteJamani, hivi mchungaji Mtikila yuko wapi? Mbona hatujamsikia kwenye swala la mchakato wa uanzishwaji wa katiba mpya? Au kahamia sisiemu?
ReplyDeleteMhe. Dada Nameloku ajaribu kuwapa semina wasichana wa kisasa na Ki mjini kuuezni utamaduni wetu badala ya kuingia ktk utumwa wa mavazi ya Magharibi!
ReplyDeleteWewe mtoa maoni wa 3 kutoka juu unaetaka kupewa mawasiliano kumfikia Nameloku Sokoine,,,,utaweza kumuuwa kwa mkuki siyo bunduki mnyama Simba? ....kwa Wamasai hilo ndio shariti namba moja kabla hata hujapeleka barua ya posa!
ReplyDeletemara yangu ya kwanza kuona Padri Mmasai. Wenzetu hawa ni washika mila wakubwa na suala la wake wengi ni kati ya mila hizo. Hata marehemu Sokoine alikuwa na wake wawili pamoja na kwamba alikuwa mkatoliki safi.
ReplyDeleteWe mdau unayeuliza kama ameolewa tafuta miwani. Yaani hujaliona hilo 'gurudumu' la nguvu kwenye kidole katika picha hiyo ya juu?
ReplyDelete