Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Kama tumekubaliana kwamba katiba ni sheria mama ya nchi na kwamba Bunge ndio chombo cha kutunga sheria, basi ni ukichaa kumpa mamlaka Rais wa nchi kusimamia mchakato wa kuunda katiba ya nchi. "Infwakti", huko ni kuingilia kazi halali ya Spika wa Bunge na Bunge "tukufu".

    Of course, unless wabunge wenyewe na Spika wao wawe bora liende na ambao hawajui misingi ya kazi yao...kama wale waliojaa pale Idodomya

    ReplyDelete
  2. Michuzi,

    This is really sad. Ms. Mwalimu doesn't understand what she is talking about. The problem is not Kamati, but how are those members going to be selected. Instead of rebutting what Lissu proposed, she wasted a lot of Bunge's time preaching to the choir.

    Comparing Kenya's Kamati with ours is like comparing apples and oranges! I am urging members of parliaments from both sides of the aisle, to be patriotic and accept constructive criticism.

    ReplyDelete
  3. Ndiyo, katiba isiishie kunadi kuwa mwanamke ana haki. Iende mpaka itoe adhabu kwa atakayewabagua.

    Pia sheria isiishie kwa wanawake tuu, iende hata kutoa adhabu kwa wabaguzi wa kabila, rangi na dini.

    Kunadi kuwa hakuna ubaguzi ni kuupa muda wa kukua ubaguzi/ukandamizi uliopo.

    ReplyDelete
  4. huyo waziri hana jipya,anatetea nafasi yake.anachoongea hakijui.Tanzania inaendelea kuchakachuliwa na wachache ahadi kila siku ambazo hazitekelezwi.Tunataka katiba nzuri mpya ambayo itatokana na watanzania wote.

    ReplyDelete
  5. sioni cheche wala baruti

    ReplyDelete
  6. Mzee hapa hakuna cheche yoyote. Upeo wa uelewa wake juu ya masuala ya katiba ni finyu mno. Ukweli kwamba nchi alizotaja zilikua na tume inayofanana na hii ambayo serikali inataka itumike haulazimishi Tanzania kufuuata. Mheshimiwa haelezi kama athari ambazo wapinzani na watanzania wengi wanazozizungumzia zilipata kuwapo huko ama la. Yeye anaishia kusema tu utaratibu huo ndo umezoeleka. Hatufanyi mambo kwa mazoea mabaya.Anapaswa aache kukariri. Hayo ndo matatizo ya wasomi wetu wengi hawana uwezo wakupambanua mambo kwa upana wake mkubwa. Wanaishia kuwa-descriptive tu. Narudia tena hakuna cheche hapo. Anatetea maslahi ya nafasi yake zaidi ya maslahi mapana ya watanzania ambao wanapinga mswaada huo.

    ReplyDelete
  7. Anaongea kama nani? Mwenyekiti wa tume. Mbona anaonyesha yuko soo touched, na yeye ana interest gani na Rais kuunda tume??

    ReplyDelete
  8. SEMA UMMY WALA USIOGOPE.

    KATIBA TUNAANDAA KWA MANUFAA YA TAIFA ZIMA BILA ITIKADI YA CHAMA CHOCHOTE. HIVYO WENYE NAFASI KTK BARAZA LA MAAMUZI MSIKAE KIMYA..SEMENI TENA SANA. MAJADILIANO YA PAMOJA NI NGUVU ZA WANANCHI WALA SI KUCHOMA MATAIRI BARABARANI.

    VITI MAALUM VIJANA, WAFANYAKAZI, NGO BADO HATUJAWASIKIA. MSIJE MKATETA NJE YA BUNGE. HUMO NDIO LAZIMA KIELEWEKE, MSIWAACHIE WAHAFIDHINA WA CONSERVATIVE NA REPUBLICAN WATANUE MISULI YAO BUNGENI KWA NJIA YA DEMOKRASIA NA MAENDELEO.

    MAINA A. OWINO

    ReplyDelete
  9. Wewe mwanamke tafadhali usiongee kwa maslahi binafsi au ya jinsia yako maana unazungumzia sana haki ya mwanamke ili upate kuungwa mkono na wanawake wenzako, lakini ujue Suala la Katiba haligusi haki ya Mwanamke tu bali linagusa haki ya kila Mtanzania bila kujali jinsia awe mtoto au mkubwa kiumri. Kwa ujumla wewe inaonekana unatetea maslahi yako na Chama chako. Lakini ujue kuvurunda kwenye Suala la Katiba kutakuathiri hata wewe familia yako, hata kizazi chako kijacho. Kinacholalamikiwa na wana harakati naona hujakielewa pamoja na usomi wako. Na napenda kukueleza hakuna sababu ya kutoa mfano Uganda, Kenya wala nchi nyingine yeyote kwani Watanzania hatuendeshwi kwa mifano bali kwa taratibu zetu zinazoweza kutupeleka kuwa na Katiba Bora hata ya hizo nchi ulizotolea mfano.
    NARUDIA NA KUSISITIZA SUALA LA KATIBA LISIFANYWE KAMA USHABIKI WA KISIASA KWANI ATHARI ZAKE ZINAWEZA KUHARIBU MAISHA YA WATANZANIA WOTE NA KUZUA BALAA KUBWA HUKO TUENDAPO. NANYI MLIO MADARAKANI MSIDHANI KWA MATAKWA YENU NDIO MTAWAFANYA WATANZANIA MILIONI 40 WAJINGA KIASI CHA KUWABURUZA MNAVYOTAKA. MTASABABISHA KUHARIBU MAISHA YENU NA YA KIZAZI CHENU KIJACHO KWA KUJALI MASLAHI YENU BINAFSI YA MUDA MFUPI WA MAISHA MTAKAYOISHI DUNIANI.

    ReplyDelete
  10. HIVI SISI WADAU TUNAOCHANGIA,..JE SISI TUMESHIRIKI VIPI SO FAR KATIKA KUTOA MAONI YETU KUHUSU KATIBA MPYA??
    AU TUNAONGEA TU KAMA KAWAIDA YA WABONGO, HUTUSHIRIKI KWA VITENDO.
    TUKUMBUKE HILI NI JAMBO KUBWA SANA KATIKA HISTORIA YA NCHI, HERI KATIBA ICHELEWE TUFIKIE MUAFAKA THABITI WA KATIBA NZURI NA YA HAKI.
    TUSHIRIKI TAFADHALI!!!

    ReplyDelete
  11. We Maina Owino acha ushabiki usio na msingi! Waache waTz, wenye uchungu walizungumzie hili suala la katiba, we ungekuwa mzalendo ongehama Tz na kwenda kulowea Ughaibuni? Hata hujui machungu ya walalahoi wa Tanzania tulio wengi. Kimsingi hatuwezi kufanya mambo kwa kukariri bwana, tunatakiwa tuchukue mazuri tu ya hizo Katiba za nchi nyingine ili zitupe muungozo na siyo kudesa! Sisi tunatakiwa tuje na utaratibu mpya unaofaa kwa nchi yetu, Kenya haiwezi kuwa sawa na Tz, Uganda pia, hata nchi nyingine yoyote ya Afrika! Wabunge wa ccm ni wavivu wa kufikiri, acha vichwa vinavyochaji vifanye kazi bwana, acheni ushabiki wa kisiasa usio na msingi! Huyu Ummy hajatema cheche wala nini, ameonyesha ufinyu wake wa kujua mambo, awe anachambua mambo kabla ya kuanza kurap kama mwanamuziki!Maina na wenzio wa ccm mtajibeba, hatumtaki rais ndiye aunde tume, kwa nini hiyo kazi asiachiwe Spika na bunge lake kwa kuwashirikisha wananchi? Huyo mkuu wa kaja kwa sasa hatumuamini kabisa yaani, akae akijua, amechoka mbaya! Uncle Michu usinibanie comment yangu tafadhali, issue ya Katiba ni muhimu sana hasa kwa sisi watz walalahoi, hatuna uwezo na kukimbilia ughaibuni kama kina Maina, basi tunabanana Tz kimtindomtindo tu,issue ya katiba inatugusa sana

    ReplyDelete
  12. Hongera Mbunge kwa maoni yako mazuri. Wananchi wote kwa ujumla inabidi wawe makini katika suala zima la Katiba Mpya ya Nchi. Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  13. huyu mama hajui ankiongea no bora angenyamaza badala kujizalilisha kama hivi,anafikiri anahutubia watu wasiojua wanachokifanya

    ReplyDelete
  14. Nchi anazozitaja hazina katiba ambayo inaweza kuigwa na watanzania.Tunaona Mseveni anavyonyasa wapinzani.Hii inadhihirisha namna viongozi wetu hawana political will,ili kuweza kuwaletea watanzania maendeleo.Vilevile wana uelewa mdogo juu ya mambo yanayotukia duniani.Ndo maana nchi inaendelea kudolola kiuchumi na asilimia 90 ya watanzania waishi chini ya dola moja.

    ReplyDelete
  15. Bra, bra bra braaa! bra Uganda, bra Kenya, bra Zambia, bra Ghana. Braaaa! Wanawake, wanaume, watoto, wasichana, braaaaaaa! Yes, braa, tume braa, commission braaaaaa!!!!
    Tanzania braaa, bra, braa, sheria zinazomyanyasa braa, br br br br. Braaaaaaa.

    ReplyDelete
  16. DUH MIMI NILIKUWA NAZANI KUWA MCHAKATO WA KATIBA NDIYO UNAKWISHA, NILIKUWA NAPINGA TU. KUMBE KINACHOONGELEWA NI KUUNDWA TUME YA KURATIBU UKUSANYWAJI WA MAONI!!!!

    DUH SASA ITABIDI VYAMA MBADALA VIFANYE KAZI YA ZIADA YA KUNIELEZA KWANINI HATAWATAKI SHERIA ZILIZOPO SASA ZISIFANYE KAZI YA KUHAKIKISHA TUME INAUNDWA NA SISI WANANCHI TUPATE WASAA MWAFAKA WA KUTOA MAONI.

    NIMEMSIKILIZA HUYU MBUNGE LEO NDIYO NIMEELEWA NA SINA HAJA YA KUPINGA KWANINI NDIYO TUNATAYARISHIWA TUME ITAKAYOKUSANYA MAONI KUTOKA KWETU WANANCHI. SAFI SANA NINAWAUNGA MKONO SPIKA. HAKIKISHENI MNATOA ELEMU YA KUTOSHA WENGINE ZAIDI WAWEZE KUELEWA NA MSIKUBALI MCHAKATO WA KUTUFIKIA WANANCHI UCHELEWESHWE KWA SABABU BINAFSI.

    ReplyDelete
  17. Tatizo watu wakiwa katika nafasi, basi wanasahau nafasi za chini. Hawafikirii kuwa hakuna marefu yasiyokuwa na ncha. Wakumbuke kuwa ipo siku watatoka katika nafasi hizo, hayo wanayoshupalia baadaye yatakuja kuwagonga. Waziri anajupendekeza tu aweze kuendelea katika nafasi. Lakini hauchi hauchi utakucha tu.

    Hakuna cheche hapo, ni ufinyu wa mtazamo.

    ReplyDelete
  18. wote mnao lalama hapa hakuna hata mmoja wetu mwenye uchungu wa kweli kazi yetu nikutoa maoni mazito lakini hata moja wetu hana dhamira ya kweli nani aliyewahi kushiliki katika kutoa maoni yake kwenye vyomba husika? zaidi ya hapa nawasiwasi wengi wetu hata uhaguzi unapo fika wengi wetu hatupigi kura hayo mabadiliko tunayotaka tutayapataje? kweli na waambia kama hatutabadilika ccm itaendelea kutawala maisha(mtanganyika)

    ReplyDelete
  19. Chadema mmekwama, mnachokitaka hakita kuwa. Mnaonekana hamna hoja nyie ni haribu tu, hata tuliokuwa njia panda sasa njia tumeiona looh hamna haya nyie wala hamjui vibaya, mna mchukia mtu mpaka mnashindwa kujizui............urais sio kikwete, urais ni taasisi na taasisi zina mipangilio yake, obviously hili hamlitambui mnatambua fuja, maandamano n.k Yule bwege wenu wa Arusha anafikiri yeye bado misheni town msela wa kijiweni kajisahau kuwa yeye sasa ni mbunge na anawakilisha wananchi wote wa jimbo lake si waendesha mapikipiki na madala dala tu, ambao ndio aliokuwa anakaa nao kijiweni.

    ReplyDelete
  20. Nafikiri elimu ya ziada inatakiwa kutolewa kwa watanzania kuhusu hili swala kabla ya kuanza kuchukua hayo maoni kutoka kwao. kwa watu wengi sana nchini hawana uelewa kabisa na yaliyomo kwenye katiba sasa je watachangia maoni gani? Watu huishia tu kusema katiba hii ni mbaya ndo maana maisha magumu..! sawa yawezekana, lakini ukimuuliza ni vipengele vipi haswa unavyofikiri vinahitaji kurekebishwa haelewi chochote. Kweli hili jambo sio la kufanya haraka serikali ichukue muda wa kutosha kabla ya kufikia maamuzi. Pole JK huu ndio muda wa kutumia busara kuliko wakati wowote wa kipindi chako cha utawala. Mungu saidia Tanzania.

    ReplyDelete
  21. AJUI CHOCHE ANACHOKIONGEA KABSA,...BRA BRAAAAAAAA

    ReplyDelete
  22. Eti "Na mimi nilikuwa mwanaharakati; kuna interest za watu behind" Ndio shida ya kuongea sana. Huoni kuwa unajidharirisha na wewe? Haya tutakuwaje na uhakika kuwa na hilo unalopigania hakuna "interest behind?" Maana umeshakiri kuwa huko tayari ku engage na unethical business as long as mkono unaingi kinywani.

    ReplyDelete
  23. MABADILIKO YA KATIBA NI LAZIMA KUFUATIA KIGEZO CHA KWANZA:::::RAISI WA TANZANIA KUWA NA MAMLAKA KAMA MWENYEZI MUNGU!...hakuna nchi ktk sayari ya dunia tunayoishi ambayo haya yanayojiri kwetu yapo isipokuwa hapa kwetu,,,hii ni hatari sana!!!!

    ReplyDelete
  24. Mlitaka katiba ilipotaka kuletwa kwa haraka mkazuuya sasa mnaanza visingizio.
    Mnacheza na Kikwete atawapeleka mbio mpaka mtajuta mlidhani ana beep kumbe anapiga maskini sas mambo magumu kwenu.

    ReplyDelete
  25. TUME YA KURATIBU MAONI YA KATIBA ITATOKANA NA WABUNGE NA SIYO RAIS NDIYO ISSUE KUBWA HAPA..!

    ReplyDelete
  26. ACHENI NINYI WASHAMBA HUYO DADA KAMA KIONGOZI NI MWANAMKE WA SHOKA KWANI WANAWAKE WAMESAHAULIKA SANA NA HAWANA HAKI HATA KIDOGO KATIKA JAMII YETU TANZANIA ! MUACHENI APIGANIE HAKI YA MWANAMKE , AU KWA SABABU SISI WATANZABNIA TUMEZOEA KUWAZALILISHA WANAWAKE HATA WAUME ZAO WANAPOFARIKI HUFUKUZWA KWENYE NYUMBA ZA WAUME ZAO KAMA MBWA KWA SABABU HAWANA HAKI ETI HATA KAMA KAZAA NA MUMEWE ANAONEKANA KAMA KINYAA, HUO NDIO MWANZO WA SAUTI YA KIKE KATIKA JAMII NA SIKU MOJA WATAKUWA VIONGOZI BORA HATA KUWA MARAIS.

    HONGERA DADA UMMY ALUTA KONTINUA

    ReplyDelete
  27. weye anony Tue Nov 15, 10:53:00 PM 2011: yaaani wote aliyekukuna ni Maina Owino; mbona kila mara tunaye kwenye miradi ya vijijini sasa kukimbilia ughaibuni na kukosa uchungu kuna toka wapi au mtimanyongo tu>?.

    Nimerudia comments zake mara kadhaa sioni kanyambala wapi au urafiki wenu umekong'ola pili pili. Kazidi kushawishi wabunge wote bila itikadi waseme na sio kumbeya nje ya bunge, kwa kuwa ni maina owino wa ccm baaaasi kajalala.

    Mjifunze kuvumiliana kwa mawazo. kwe!
    Deus Mwakasukwa.
    MBEYA.
    CHADEMA OYEE

    ReplyDelete
  28. Naomba niwaombe wachangia mada wasiwe na jzba kwa aina mama.. inanekana dhahiri kuwa wana mawazo mgando kwa kuongelea mambo ya braaaa..
    Nionavyo na sisi tunakuwa kama waheshimiwa wabunge, unaacha ya maana nakukejeli jinsia....
    cha msingi ni bora tutoe maoni ya vipengele vinahitaji maboresho gani... masuala ya demokrasia za jazba hayatatupeleka mbali, tusonge mbele tusirudi nyuma , tutajikuta muswada tnadai usomwe hata mara 20... pole zetu WaTZ tutabaki nyuma tu.... Jasmin

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...