Mlinzi wa timu ya taifa ya Zanzibar, Makame Hamad (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa Uganda, Dan wagaruka wakati wa mchezo wa ufunguzi wa michuano ya kombe la Chalenji uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Uganda ilishinda 2-1.
Beki wa Uganda, Adrew Mwesigwa akijaribu kumzuia mshambuliaji wa Zanzibar, AQli Badru Ali.
Golikipa wa timu ya taifa ya Zanzibar, Mwadini Ali Mwadini akiruka juu kuokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.Picha na Francis Dande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Sijui macho yangu mabovu. Lakini nionavyo ni kama wachezaji wamevaa viatu vya rangi tofautitofauti. Hii ilikuwa mechi ya mchangani au ni michuano mikubwa ya chalenji????

    ReplyDelete
  2. hao hawafiki kokote washazoea kula urojooooo

    mdau Gida

    ReplyDelete
  3. wewe anony wa kwanza inaonekana hujui kabisa mpira na ni zumbukuku, watu kama wewe huwa tunawaita washamba na wenye viherehere..kupata jibu kwa nini nakwita wewe ni bongo lala kwenye michezo tena hasa soka..tafuta picha zote za vikosi vya timu zilizoshiriki kombe la dunia maana hilo ndo kubwa kuliko lolote ktk soka, alafu uangalie kama wachezaji huvaa viatu sawa ama sare..nyamafu we! ingia mjini vizuri wewe....

    ReplyDelete
  4. kuhusu suala la viatu kuwa na rangi tofauti ni kawaida mdau,angalia mechi yoyote katika michuano yoyote duniani hutaona wachezaji wamevaa viatu vya rangi moja.jezi na soksi tu ndo lazima zifanane.

    ReplyDelete
  5. we mdau hapo juu sio mwana michezo nn???? rangi ya viatu haina ishu kwenye mpira, angalia ligi za nje na waangalie viatu, acha ushamba wa kizamani wewe!!!!

    ReplyDelete
  6. urojo lakini ndio wanofika mbali kuliko wanokula sembe,ama kuh.viatu siku hizi wachezaji wanavaa kila kiatu rangi yake mtu mmoja tu

    ReplyDelete
  7. Kwani mngemuambia tu kuwa rangi za viatu zaweza kutofatiana kati ya mchezaji mmoja na mwingine wa timu moja pasipo kumtukana na kumdhihaki mngepungukiwa nini mbele ya Mungu kwa kiumbe alichokiumba kwa mfano wake mwenyewe??? Kwa nini mnapenda shetani awatangulie namna hiyo???

    ReplyDelete
  8. Naona poulsen arudi kwao heri ya maksimo bwana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...